Habari kwa mujibu wa Mohamed
Hamad, Kiteto -- WILAYA ya Kiteto
imeingia kwenye orodha ya maeneo
yanayotisha kwa mauaji ya kinyama
baada ya wakulima kuuawa mara kwa
mara na wafugaji kutokana na sababu
mbalimbali zikiwemo za kugombea
ardhi
Miongoni mwa waliouawa kinyama
Dec 20 kwa kuchinjwa shingo yake ni
Juma Mlagwa (49) wa Kitongoji cha
Kalikala Kata ya Njoro (Kiteto) ambaye
alivamiwa nyumbani kwake usiku na
kundi la vijana wa kifugaji masai
(makorianga)
Imeelezwa kuwa wakati anavamiwa
zilisikika Risasi zikipigwa juu
Kitongojini hapo na baada ya watu
kuendelea kujificha ndani vijana hao
walianza kunyunyizia nyumba zao
mafuta aina ya petrol kisha kuwasha
moto
Akizungumza mbele ya Mkuu wa
Mkoa wa Manyara Ally Mussa
Mwenyekiti wa Kitongoji hicho
alisema siku hiyo haitasahaulika
mashani mwake kwa yaliyotokea
kutokana na vitendo hivyo akisema
ilikuwa mara ya kwanza kuona mtu
anachinjwa hadharani
“Nilichomewa Pikipiki zangu mbili
pamoja na vitu mbalimbali vya ndani
zikiwemo nguo, vyakula, lakini
nilichonusuru ni roho yangu ambayo
hadi leo nasema najivunia uhai nilio
nao”alisema Mwenyekiti huyo
Alisema chanzo cha mauaji hayo ni
jamii ya kifugaji wamasai kuingiza
mifugo yao kwenye shamba la mmoja
wa wakulima Kitongojini hapo na
baada ya kukatazwa walimpiga kisha
nae kupigwa ndipo wakakusanyana
kupanga uvamizi huo
Hata hivyo baada ya kufikishwa
taarifa kwa viongozi wa Serikali
walidaiwa kulifika Kitongojini lakini
walikataa kwenda kuongea nao km
chache kwa madai kuwa ni uongo
kwamba hakuna watu
waliokusanyana
Akielezea hayo Mwenyekiti huyo
alisema tatizo ni uongozi dhaifu
kuanzia ngazi ya Kitongoji hadi Wilaya
ambapo alidai kuwa ukabila
umeshamiri kwa viongozi kujiona
kuwa wanahaki ya kutfanya utetezi
katika upande mmoja
Kwa upande wake Lairumbe Mollel
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Wilaya akizungumzia sakata hilo
alimzodoa mwenyekiti huyo wa
Kitongonji kuwa ni muongo kwani
baada ya wao kufika kabla ya tukio
alikataa kuwataja wahusika
Hata hivyo kauli hiyo ilionekana
kutokuwa na mashiko baada ya
mwenyekiti huyo wa Kitongoji
kuonyesha udhaifu wa viongozi hao
akisema baada tu ya kufika
hawakuweza hata kukubali kupelekwa
walikoweka kambi vijana hao wa
kimasai
“Baada ya kufika walitaka nisema
majina ya walioleta fujo na
nilipowataka twende eneo la tukio
wakakata nakuona kuwa hawakuwa
na njia njema kisha wakarejea Kiteto
ambapo usiku vijana hao
wakatekeleza azima yao ya kuchinja
mtu mmoja na kumpiga mwingine
risasi kisha kuwajeruhi watu
saba”alisema Mwenyekiti huyo wa
kitongoji
Waliofariki katika uvamizi huo ni
pamoja na Juma Malagwa (49)
ambaye alichinjwa shingo, Yohana Ivo
(33) ambaye alipigwa sehemu
mbalimbali za mwili na kusababisha
kifo pamoja na watu wengine saba
kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya
Kiteto kwa kujeruhiwa kwa fimbo na
mapanga
Waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya
ya Kiteto ni Hoti Daniel (38) Emanuel
matias (21) Juma Bahati (13)
Mwajuma Hamisi (20) Habiba Ally (16)
Mwajuma Martin pamoja na Musa
Juma (16) aliyepelekwa Dodoma
kwaajili ya matibabu
Hata hivyo mkuu huyo wa Mkoa wa
Manyara Elaston Mbwillo akiwa katika
kitongoji hicho aliwapa siku 30
viongozi wa Wilaya ya Kiteto kuweka
utaratibu wa kuwatambua wananchi
hao ili kuondoa tofauti zao waweze
kufanya kazi bila bughdha
“Ninyi wananchi mwende kujisajili
Kijijijini ili Serikali iwatambue kwani
maisha bora kwa wananchi
yatapatikana kwa kufahamika mlipo ili
mpatiwe huduma za jamiiambazo kwa
sasa hamna hata moja,” alisema
Mbwillo.SAMAHANI PICHA YAKE INATISHA ,KAMA UNAUJASIRI BONYEZA HAPA USOME.
Hamad, Kiteto -- WILAYA ya Kiteto
imeingia kwenye orodha ya maeneo
yanayotisha kwa mauaji ya kinyama
baada ya wakulima kuuawa mara kwa
mara na wafugaji kutokana na sababu
mbalimbali zikiwemo za kugombea
ardhi
Miongoni mwa waliouawa kinyama
Dec 20 kwa kuchinjwa shingo yake ni
Juma Mlagwa (49) wa Kitongoji cha
Kalikala Kata ya Njoro (Kiteto) ambaye
alivamiwa nyumbani kwake usiku na
kundi la vijana wa kifugaji masai
(makorianga)
Imeelezwa kuwa wakati anavamiwa
zilisikika Risasi zikipigwa juu
Kitongojini hapo na baada ya watu
kuendelea kujificha ndani vijana hao
walianza kunyunyizia nyumba zao
mafuta aina ya petrol kisha kuwasha
moto
Akizungumza mbele ya Mkuu wa
Mkoa wa Manyara Ally Mussa
Mwenyekiti wa Kitongoji hicho
alisema siku hiyo haitasahaulika
mashani mwake kwa yaliyotokea
kutokana na vitendo hivyo akisema
ilikuwa mara ya kwanza kuona mtu
anachinjwa hadharani
“Nilichomewa Pikipiki zangu mbili
pamoja na vitu mbalimbali vya ndani
zikiwemo nguo, vyakula, lakini
nilichonusuru ni roho yangu ambayo
hadi leo nasema najivunia uhai nilio
nao”alisema Mwenyekiti huyo
Alisema chanzo cha mauaji hayo ni
jamii ya kifugaji wamasai kuingiza
mifugo yao kwenye shamba la mmoja
wa wakulima Kitongojini hapo na
baada ya kukatazwa walimpiga kisha
nae kupigwa ndipo wakakusanyana
kupanga uvamizi huo
Hata hivyo baada ya kufikishwa
taarifa kwa viongozi wa Serikali
walidaiwa kulifika Kitongojini lakini
walikataa kwenda kuongea nao km
chache kwa madai kuwa ni uongo
kwamba hakuna watu
waliokusanyana
Akielezea hayo Mwenyekiti huyo
alisema tatizo ni uongozi dhaifu
kuanzia ngazi ya Kitongoji hadi Wilaya
ambapo alidai kuwa ukabila
umeshamiri kwa viongozi kujiona
kuwa wanahaki ya kutfanya utetezi
katika upande mmoja
Kwa upande wake Lairumbe Mollel
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Wilaya akizungumzia sakata hilo
alimzodoa mwenyekiti huyo wa
Kitongonji kuwa ni muongo kwani
baada ya wao kufika kabla ya tukio
alikataa kuwataja wahusika
Hata hivyo kauli hiyo ilionekana
kutokuwa na mashiko baada ya
mwenyekiti huyo wa Kitongoji
kuonyesha udhaifu wa viongozi hao
akisema baada tu ya kufika
hawakuweza hata kukubali kupelekwa
walikoweka kambi vijana hao wa
kimasai
“Baada ya kufika walitaka nisema
majina ya walioleta fujo na
nilipowataka twende eneo la tukio
wakakata nakuona kuwa hawakuwa
na njia njema kisha wakarejea Kiteto
ambapo usiku vijana hao
wakatekeleza azima yao ya kuchinja
mtu mmoja na kumpiga mwingine
risasi kisha kuwajeruhi watu
saba”alisema Mwenyekiti huyo wa
kitongoji
Waliofariki katika uvamizi huo ni
pamoja na Juma Malagwa (49)
ambaye alichinjwa shingo, Yohana Ivo
(33) ambaye alipigwa sehemu
mbalimbali za mwili na kusababisha
kifo pamoja na watu wengine saba
kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya
Kiteto kwa kujeruhiwa kwa fimbo na
mapanga
Waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya
ya Kiteto ni Hoti Daniel (38) Emanuel
matias (21) Juma Bahati (13)
Mwajuma Hamisi (20) Habiba Ally (16)
Mwajuma Martin pamoja na Musa
Juma (16) aliyepelekwa Dodoma
kwaajili ya matibabu
Hata hivyo mkuu huyo wa Mkoa wa
Manyara Elaston Mbwillo akiwa katika
kitongoji hicho aliwapa siku 30
viongozi wa Wilaya ya Kiteto kuweka
utaratibu wa kuwatambua wananchi
hao ili kuondoa tofauti zao waweze
kufanya kazi bila bughdha
“Ninyi wananchi mwende kujisajili
Kijijijini ili Serikali iwatambue kwani
maisha bora kwa wananchi
yatapatikana kwa kufahamika mlipo ili
mpatiwe huduma za jamiiambazo kwa
sasa hamna hata moja,” alisema
Mbwillo.SAMAHANI PICHA YAKE INATISHA ,KAMA UNAUJASIRI BONYEZA HAPA USOME.