Wanjeshi wa Ufaransa wanaendesha msako ndani ya gari, huko wanajeshi wa Seleka wakipiga doria mjini BaguiREUTERS/Andreea Campeanu
Na
RFIWanajeshi wapatao watano wa Tchad wa kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Misca wameripotiwa kuuwawa katika makabiliano makali dhidi ya wapiganaji wa anti-balaka katika wilaya ya Gobongo. Aidha, wanajeshi wa Ufaransa wanaonekana kuzidiwa na vurugu hizo kubwa na kutangaza kuongeza ushiriki wake wa kijeshi ikiwa hali itaendelea kuwa tete.
Mkurugenzi wa zamani wa Chuo cha kijeshi na mtaalam wa masuala ya ulinzi wa kimataifa Sayansi ya kisiasa kwa nchi zinazozungumza Kifaransa, Jenerali Vincent Desportes, amesema hali ya mjini Bangui inakua tete zaidi, kuna ulazima kupitia upya aidha kurekebisha plani ya awali, akibaini kwamba idadi ya wanajeshi wa ufaransa inapashwa kuongezwa kwa sababu wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Afrika Misca wazidiwa na hali ilivyo kwa sasa.
Kwa upande wake, mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kwa ajili ya kuzuia mauaji ya kimbari, Adama Dieng ameelezea wasiwasi wake kwa machafuko yanayoendelea nchini jamhuri ya Afrika ya kati na kuunga mkono jitiada za vikosi vya kimataifa vya kupokonya silaha.
“Naomba niseme kwamba kulingana na machafuko yanayoendelea bila uwajibikaji, Jamuhuri ya Afrika ya Kati inawez kugeuka dimbwi la mauwaji ya kutisha, lazima kuchukuliwe hatua za haraka na watuhumiwa wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria”, amesema Dieng.
Nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati, kunaendelea kushuhudiwa machafuko, baada ya waasi wa Seleka kumn'goa madarakani alie kua rais wa nchi hio Bozize.
Kwa sasa vita vya kidini vinaendelea kushuhudiwa nchini humo.