Machar akutana na mjumbe wa Marekani



Taarifa ya waasi wa Sudan Kusini inasema kuwa mjumbe wa Marekani, Donald Booth, pamoja na wapatanishi wa kanda ya Afrika Mashariki, wamezungumza na kiongozi wa waasi hao, Riek Machar.
Taarifa hiyo iliyopokewa na shirika la habari la Ufaransa ilieleza kuwa mazungumzo hayo yalifanywa Jumamosi lakini haikutaja yalifanywa wapi.Taarifa imetiwa saini na Miyong G Kuon, afisa wa habari wa Bwana Machar.
Hakuna mtu mwengine aliyethibitisha habari hizo.
Mazungumzo ya amani nchini Ethiopia ambayo yanalenga kumaliza majuma mane ya vita nchini Sudan Kusini hayaoneshi kuwa yamepiga hatua.
Inaonekana kizuiizi kikubwa ni shuruti ya Bwana Machar kuwa wafuasi wake 11 waachiliwe huru mjini Juba.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company