CCM WASHINDA KATA ZOTE TATU MKOA WA IRINGA, CHADEMA YASHINDA NJOMBE MJINI,ARUSHA CHADEMA WANYAKUA IKIWEMO SOMBETINI LEMA APIGWA NA POLISI



Wafuasi wa CCM Iringa wakimpongeza kaimu katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga kwa kufanikisha chama hicho kushinda uchaguzi mdogo kata ya Nduli.

Wafuasi wa CCM kata ya Nduli wakiwa wamemnyanyua juu juu aliyekuwa mgombea udiwani kata ya Nduli Bw Mtove baada ya matokeo kumpa ushindi wa kishindo leo
...........................CHAMA cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kimefanikiwa kutetea kata zake zote tatu ambazo leo wananchi wameshiriki kupiga kura kuwachagua madiwani kufuatia nafasi hiyo kuwa wazi baada ya madiwani wake kufariki dunia.

Wafuasia wa CCM walimpongeza aliyekuwa mgombea wa CCM kata ya Nduli pamoja na kaimu katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga na kudai kuwa kazi yake inaonesha wazi safari yake ya kulitwaa jimbo la Iringa mjini.


Matokeo katika vituo vyote tisa ambavyo wananchi wa Nduli walipata kuvitumia kupiga kura ,kituo cha Mawasiliano CCM (57),Chadema(28),Zahanati CCM( 114), Chadema ( 47), Shule Nduli CCM(70) Chadema(39), KIngonzile shule CCM(105) Chadema(82),Mibata CCM(48) Chadema(103), MTalagala CCM(95),Chadema(54),Godauni CCM(138 ,Chadema(52),Njiapanda CCM (75) Chadema (52),Msisina CCM (156 ) Chadema (31)

Katika Matokeo hayo ambayo hadi sasa majira ya saa 12.50 bado msimamizi wa uchaguzi kutangaza CCM inaongoza kwa kura 854 huku hadema wakifuatia kwa kura 487,Mbali ya matokeo hayo ya kata ya Nduli pia CCM imeshinda kata ya Ibumi na Ukumbi zote za wilaya ya Kilolo.

Katika kata ya Njombe mjini mgombea wa Chadema amembwaga mgombea wa CCM ambapo matokeo yanaonyesha mpinzani wake ameongoza katika kituo kimoja pekee kwa tofauti ya kura 2 huku katika vituo vyote Chadema ikiibuka kidedea.

ARUSHA...
CHADEMA wameshinda  Kata ya Sombetini kwa 2548 na CCM 2077, Kiboriloni ya Mjini Moshi na Njombe Mjini Mkoani Njombe. Matokeo yote utayapata hapa. Usiwe mbali tafadhali.
Sanduku la Kura
Kata ya Kasanga Mkoani Rukwa wanaongoza na wameshinda pia Kata ya Kiomoni Mkoani Tanga  
. Na mbunge wa jimbo la Arusha Mjini G Lema amepigwa na polisisi wa kutuliza gasia leo alasiri eneeo la kona ya Mbauda baada ya kuongoza ushangiliaji uliosababisha kufungwa kwa muda kwa barabara.Akihohjiwa na SUNIRISE radio amesema "Polisi wamenipiga hadi nikajifanya nimekufa walipotaka kunipeleka mochwari nikazinduka"alisema hivyo                
KABLA NA BAADA YA MATOKEO YA UDIWANI ARUSHA KUTOLEWA CHEKI PICHA












 www.hakileo.blogspot.com
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company