Marekani yatahadharisha kuhusu uvunjwaji wa makubaliano ya kusitisha vita nchini Sudani Kusini


Jen Psaki,msemaji wa Idara ya Marekani
AFP Photo/Paul J. Richards
Na Sabina Chrispine Nabigambo
Marekani imetoa tahadhari kuhusu madai ya mara kwa mara kwamba serikali ya Sudani Kusini na waasi wanavunja makubaliano ya kusitisha mapigano ambyo yamegharimu maisha ya maelfu ya watu.
Waangalizi wa mpango huo wa kusitisha mapigano, wamepelekwa nchini humo juma hili huku kukiwa na mapigano ambayo yanaendelea licha ya makubaliano yaliyotiwa saini mwezi uliopita na serikali ya Juba na waasi, chini ya (IGAD).

Msemaji wa Idara ya Marekani Jen Psaki amesema katika taarifa kuwa Marekani ina wasiwasi na taarifa za ukiukwaji wa makubaliano yaliyofikiwa na serikali ya Sudan Kusini na majeshi ya kupambana na serikali mnamo Januari 23,kuhusu kukomesha uhasama na umwagaji damu.

Aidha ametoa wito kwa serikali ya Sudani kusini kuwwasaidia waangalizi wa utekelezaji wa makubaliano hayo kufanya kazi hiyo muhimu ili kuruhusu pande zote mbili kuarifu kuhusu uvunjwaji wowote wa makubaliano.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company