Taliban wajigamba na Mbwa wa Marekani


Mbwa aliyekamatwa laikuwa anatumiwa 'na kikosi maalum cha jeshi la Marekani nchini Afghanistan
Kundi la wapiganaji wa Taleban limesema kuwa limemkamata Mbwa kutoka kwa wanajeshi wa Marekani Mashariki mwa Afghanistan.Picha waliyoiweka kwenye akaunti yao ya Twitter, inaonyesha Mbwa mdogo wa hudhurungi akiwa na kamba ndogo shingoni.
Taliban wanasema kuwa Mbwa huyo kwa jina, 'Kanali' alikamatwa usiku wakati wa msako uliofanywa mwezi Disemba.

Mbwa huyo alikuwa na tochi ndogo, kamera na kifaa cha GPS.

Pia walionyesha silaha walizonasa wakati wa msako huo, ambazo hutumiwa na kikosi maalum cha jeshi la Marekani.

Mwandishi wa BBC anasema kuwa kumekuwa na taarifa za kiongozi wa Taliban katika eneo hilo kuonekana akiwa na Mbwa huyo ambaye sasa ni mfungwa wa kivita.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company