Wapenzi wa jinsia moja kuwakilishwa Afrika Kusini kisiasa,Chama chao chapeteta.


Shughuli ya kupiga kura Afrika Kusini
Chama kipya kinachowatetea wapenzi wa jinsia moja kitasimamisha wagombea nchini Afrika Kusini mwaka huu.
Msemaji wa chama hicho cha Equal Rights, Michael Herbst amesema kuwa chama hicho kiliundwa ili kuwalinda wanawake wanaobakwa na wanaume wanaodai kuwa wanataka kuwaondoa katika usagaji.Ameongezea kuwa watoto ambao wanao-newa kwa kuwa wanadaiwa kuwa wapenzi wa jinsia moja wanahitaji sauti ya kuwasaidia.

Katiba ya Afrika Kusini inapinga ubaguzi wowote kutokana na maswala ya jinsia na kwamba ndoa za watu wa jinsia moja zinaruhusiwa.

Lakini waandishi wanasema kuwa mapenzi ya jinsia moja ni mwiko katika maeneo mengi ya mashambani pamoja na yale ya mijini.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company