WHO yaonya kuhusu wimbi la Saratani


Uraibu wa pombe na sigara husababisha saratani
Shirika la Afya duniani WHO limeonya kuhusu kuibuka kwa wimbi baya la maambukizi ya ugonjwa hatari wa saratani kote duniani.Shirika hilo limesema nusu ya ugonnjwa wa Saratani yanaweza kuzuiwa na kwamba juhudi mpya zinastahili kufanyika ili kukabiliana na tatizo la kunenepa kupita kiasi, ulevi na uvutaji sigara.

Watu milioni kumi na nne wanajulishwa kuwa wanaugua saratani kila mwaka, lakini idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka na kufikia milioni ishirini na nne katika kipindi cha miongo miwili ijayo.

Taasisi ya utafiti wa kimataifa kuhusu ugonjwa wa Saratani katika shirika la WHO lilionya kuwa gharama ya matimabu inaongezeka kwa kiwango ambacho ni vigumu kumudu.

Taasisi hiyo imesema serikali zinahitajika kutekeleza sheria kali zaidi kuhusu matumizi ya pombe na sukari kama vile kuongeza bei na marufuku ya matangazo ya kibiashara ya bidhaa hizo.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company