Bendera ya Urusi inapepea kwenye majengo ya serikali katika eneo la Crimea


Wanamgambo wanaounga mkono Urusi wakipandisha bendera ya Urusi kwenye makao makuu ya jeshi la majini mjini Sébastopol. REUTERS/Vasily Fedosenko, Na RFI
Jinsi siku zinavyoenda ndivyo mchakato wa kujiunga kwa Crimea na Urusi unavyoendelea. Mahakama ya kikatiba ya Urusi imetia saini leo asubuhi ya kujiunga kwa Crimea na Urusi. Wakati huo huo, wakereketwa wa naounga mkono Urusi wamevamia makambi na maeneo mengine ya jeshi la Ukraine.Bendera ya Urusi inapepea kwa sasa katika makao makuu ya jeshi la majini la Ukraine mjini Sebastopol. Jengo hlio limevamiwa leo asubuhi na kundi la wakereketwa zaidi ya kumi na mbili wanaounga mkono Urusi, baadhi yao wamekua wamejifunika nyuso zao.

Watu hao wanabaini kwamba wa memteka mkuu wa kikosi cha wanajeshi wa majini wa Ukraine, Serguiï Gaïdouk.

Wanajeshi wa Ukraine waliondoka katika ngome yao, bila hata hivo kutokea kwa mapigano, siku moja tu baada ya rais wa Urusi Vladmir Putine kusaini sheria ya kutambua uhuru wa Crimea na kujiunga kwa kisiwa hicho na Urusi
Tangu jumapili machi 16, hali ya mambo imeendelea kubadili taswira.

Baada ya matokeo ya kura ya maoni 17 machi, ambapo raia wa Crimea walipiga kura ya kujiunga na Urusi kwa asilimia 96.

Na tangu jumatatu, bunge la Crimea lilitangaza kwamba Crimea imejitenga na Urusi na kuomba rasmi kujiunga na Urusi.

Baadae jioni, rais wa Urusi Vladmir Putin alitia saini ya kutambua uhuru wa Crimea , na jumanne 18 machi mchana, sheria ya kujiunga kwa Cimea na Urusi ikasainiwa na mataifa hayo mawili. Bunge la Moscow linasubiriwa kuidhinisha sheria ya kujiunga kwa mataifa ya Crimea na Urusi.

Umoja wa Ulaya umesema hautambui wala hautotambua kujiunga kwa Crimea na Urusi. Katika miji ya Ulaya kauli ni hio.

“Ni masikitiko makubwa kuona Urusi unakubali uamzi wa Cimea wa kujitenga na Ukraine”, amesema William Hague, Waziri huyo wa mambo ya nje wa Uingereza, amesema nchi yake itasitisha ushirikiano wake wa kijeshi na Moscow.

Ujerumani kupitia, waziri mkuu wa nchi hio, kanzsela Angela Merkel, amependekeza kuanzishwa kwa mazungumzo mapya, huku akilani mkataba “dhidi ya haki ya kimataifa”.

Kwa upande wake rais wa Ufaransa, François Hollande, kikao Umoja wa Ulaya cha hivi karibunikitakachofanyika tarehe 20 na 21 machi kitatoa fursa kwa uamzi mkali utakaochukuliwa kufuatia msimamo wa Urusi wa kukubali kujiunga na Crimea.Rais wa Marekani Barack Obama, amependekeza mkutano wa viongozi wamatifa 7 yaliyoendelea kiviwanda (G7) na Umoja wa Mataifa mjini La Haye ili kujadili hali inayojiri nchini Ukraine.

Kikao hiki, ni namna nyingine, kama inahitajika, kuonesha Urusi kwamba imekua ikijitenga kila mara peke yake katika mataifa yaliendelea kiviwanda, amesema Obama.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company