Iringa. Mgombea wa ubunge Jimbo la Kalenga kupitia Chama cha Chausta, Richard Minja atazindua kampeni zake rasmi leo.
Katibu Mkuu wa Chausta, Mwaka Mgimwa alisema pamoja na kuchelewa kuanza kampeni, watafanya kazi kubwa ili kuhakikisha wanapata ushindi katika jimbo hilo.
Alisema alikuwa bungeni Dodoma na kwamba amejipanga kufanya kampeni kijiji hadi kijiji katika muda uliobaki.
Chama hicho kimeshindwa kuanza kampeni mapema kutokana na mgombea wake kuwa nje ya mkoa kwa muda mrefu kutokana na kubanwa na shughuli za kijamii.
Chausta walitarajiwa kuzindua kampeni tangu Februari 22 katika Kijiji cha Kibaoni Kata ya Ifunda, lakini ilishindikana kwa kuwa mgombea alikuwa nje ya jimbo.
Akiongea na Mwananchi kwa njia ya simu, Minja alisema kwamba kuwa kimya haina maana kwamba, hatafanya kampeni kwenye uchaguzi huo.
“Nafanya kampeni kimya kimya, siyo lazima kusindikizwa na matarumbeta kwenda kwenye kampeni kama wanavyofanya wengine. Wao wana staili yao na mimi nina yangu,” alisema Minja.
Wakati Chausta wakisuasua kuanza kampeni, vyama vya CCM na Chadema vimeendelea kushikana mashati.
Kwa upande wao CCM, wamewataka wapinzani wao Chadema kufanya kampeni zenye taswira ya amani na utulivu kwa faida ya wananchi wa Kalenga.
Wakati CCM wanatoa kauli hiyo, Chadema wamelishukia Jeshi la Polisi wakitaka litende haki wakati wote wa kampeni ili kuepusha vurugu zisizo na ulazima.
Kauli hizo zimetolewa na viongozi wa vyama hivyo wa kitaifa waliowasili Kalenga kushiriki kampeni.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago