Wanyarwanda watatu waondolewa Afrika ya kusini


Raisi Wa Rwanda Paul Kagame
  Na RFI
Afrika ya kusini imewaondoa wanadiplomasia watatu raia wa Rwanda ikiwahusisha na shambulizi dhdidi ya makazi ya kiongozi wa zamani wa Rwanda Kayumba Nyamwasa.

Taarifa zinabainisha kuwa Rwanda nayo imeamuru kuondolewa kwa wajumbe sita wa Afrika ya kusini .

Hatua hizo zinakuja baada ya watu wenye silaha kushambulia makazi ya Kayumba Nyamwasa aliyewahi kushika wadhifa wa juu katika serikali ya Rwanda.
Hata hivyo wakati shambulizi hilo mkosoajii wa raisi Kagame Kayumba Nyamwasa hakuwepo nyumbani.

Generali Nyamwasa ameponea chupuchupu majaribio mawili ya kumuua ambapo mnamo mwaka 2010 alipigwa risasi na kujeruhiwa tukio ambalo Rwanda ilikanusha kuhusika.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company