WHO yapunguza kiwango cha sukari


Madhara ya sukari.
Shirika la Afya duniani WHO limepunguza kwa nusu kiwango cha sukari kilichopendekezwa kwa matumizi ya binadamu ili kuepusha matatizo ya kiafya kama vile kunenepa kupita kiasi na meno kuoza.
Mswada mpya wa mwongozo wa matumizi ya kila siku ya sukari umepunguza kiwango cha sukari inayopaswa kutumiwa na binadamu hadi asilimia tano ya kalori au vijiko sita vya sukari kwa siku.

WHO imesema kuwa sukari ndio chanzo cha janga la kunenepa kupita kiasi linalowahangaisha takriban watu nusu bilioni kote duniani, tatizo ambalo bado linaongezeka hususan katika mataifa yanayoendelea.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company