ABIRIA WA MIKOANI WAKWAMA DARAJA RUVU, BARABARA, DARAJA VYAJAA MAJI,FOLENI YATAWALA,POLISI WATAWALA


Wasafiri kutoka mikoani kuelekea jijini Dar es Salaam, waliokuwa wakisafiri jana wakiwa eneo la Ruvu Darajani wakitafakari jinsi ya kuvuka eneo hilo baada ya barabara kujaa maji na kushindwa kuvuka kwa mabasi kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.

Baadhi ya abiria waliamua kutembea na kuvuka kwa miguu baada ya kushushwa na mabasi waliokuwa wakisafiria katika eneo hilo, ambapo huvuka hadi upande wa pili na kupanda usafiri mwingine ambao unakuwa unageuzia eneo hilo pia.

Baadhi ya magari yaliyokwama kuvuka eneo hilo yakiwa katika msongamano huku kukiwa na usimamizi wa askari polisi.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company