
Mara kwa mara bunge hili limekuwa na mvutano kwa pande mbili amabzo moja hutaka serikali mbili huku upande mwingine ukitaka serikali tatu.
Na jana nilitamka bayana kupitia kwenye blogu hii ya kwamba nimepoteza imani na bunge hilo kutokana na mwenendo wake.
Japo wajumbe hilo wametoka ambao ni wale wa UKAWA yaani Umoja wa Katiba ya Wananchi bado bunge hilo linaendelea.
Kumbuka umoja huu unaundwa na vyama vya upinzani Tanzania na wajumbe wachache wa bunge hli ambao hutoka katika makundi maalumu.