
Mzigo ulipokamilika nyumbani kwao alipoitengenezea, Polisi wa mji huo wakamkataza kuipaisha kwa sababu ni kinyume na sheria lakini ili kuepuka kumkatisha tamaa… wakamwambia ni vyema akapata kibali kutoka kwa mamlaka ya anga.
Paul Karanja alizuiwa na polisi kuipaisha hii ndege kutoka uwanja mdogo wa ndege wa Karagita na kuwanyima uhondo zaidi ya watu 500 waliofika asubuhi ya saa 3 kuangalia chombo kikipaishwa.

Karanja ambae ni Mwalimu pia wa shule ya upili, amesema tayari ameiandikia barua mamlaka ya ndege nchini Kenya kuhusu kupaisha ndege hiyo lakini hajapata majibu.