KARUME DAY; Mauaji ya Mzee Karume acha sasa tuhoji yasiyohojika!

………the stong man in the world is the one with the best information……..
Habari hii ni kwa mujibu wa maoni ya watanzania katika mtandao wakijamii wa JAMII FORUM

Hii ni kauli ya waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Benjamin Disarel ambaye aliwahi kutawala kipindi nchi hiyo wakati wa vuguvugu la vyama vya wafanyakazi mwaka 1967, tofauti na watangulizi wake Disarel yeye aliwataka makundi yote ya waingereza wanyonge waliokuwa wanapambana kwa ajili ya maslahi yao kuwa na taarifa sahihi kwa wakati mwafaka hakika haya ni maneno mazito sana.

Naam! Leo tunapoadhimisha Karume Day kuna haja ya kuwa na taarifa sahihi kuhusu kifo cha Mzee Karume ambaye anatajwa kuwa mwasisi wa mapinduzi ya Zanzibar ya januari 12 , 1964. Nalisema hili kwa jinsi mambo yanavyofichwa nabashiri kuna uwezekano mkubwa huko mbele tuendako wazungu wakaja kutusaidia kufanya utafiti wa kifo cha shujaa huyo, ili kuelewa nayoyasema rudia makala za mwandishi nguli wa Raia Mwema Bw Joseph Mihangwa au nenda visiwani Zanzibar halafu uliza wakazi wa visiwa hivyo vya karafuu wakwambia sababu za mzee huyo kupigwa risasi mnamo tarehe7 mwezi wa 4 mwaka 1972? Kisha kwa wingi na mkanganyiko wa majibu ndio utakubaliana nami umefika wakati tuhoji yasiyohojika.

Kwanza swali rahisi hivi ni kweli serikali zetu hizi za Zanzibar na ya Muungano hazifahamu sababu za kifo cha mzee huyo? Hivi ni kweli kabisa mpaka leo tumeshindwa kuweka wazi swala hili? Kwanini? Imefika sehemu tumeruhusu mapambano na malumbano ya wanahistoria kutafiti chanzo cha mauaji hayo ilihali tumeukalia ukweli? Tunaogopa nini? kwa maana tunapojadili mauaji hayo kuna maswali na mtiririko wa kimantiki unaotushawishi kuwa mzizi haswa wa mauaji hayo ni siasa za chuki na kama tunakubaliana katika hili ni lazima twende mbele tujihoji je tumezimaliza hizo siasa za chuki? Au bado zipo?
 

Hoja ya kwanza katika mtiririko huu ni kuwa kwanza Karume hakuuawa kwa bahati mbaya la hasha! Ilikuwa ni mipango ya watu Fulani na ndio maana tunasikia matokeo yake ni kuwa baada ya kifo hicho watoto wa mzee huyo walianza kunyimwa fursa za kimaendeleo kama vile walinyimwa ajira na baadhi yao walifukuzwa kazi haya kayasema mke wa marehemu Karume mama Fatuma Karume akiongea kupitia TBC1 mwaka jana siku kama ya leo, hii ina maana kuwa baada ya kifo hiko chuki haikuisha ikahamia kwa watoto na mke wake ambaye anaweka bayana kuwa ni Nyerere tu aliyewahi kumfariji mama huyo wengine wote walimtoa kwenye kumbukumbu zao hakika hii ni chuki kubwa!

Kutokana na hali hii tunapaswa tujihoji kina nani walihusika na mauaji haya? Na nini kiliwasukuma? Na kwanini chuki hiyo ilifika kwa watoto wake? Je ikiwa bado watoto wa karume wako hai tutaaminije kuwa chuki hiyo imekwisha?
Nini mzee karume alifanya mpaka ikatokea hiyo chuki?
 Lakini tusiishie hapa kwenye mauaji haya kuna jingine , inadaiwa kuwa mzee Karume aliuwawa na mwanajeshi, je kama mwanajeshi ndiye alimwua je hayo siyo mapinduzi ya kijeshi? Kwanini? Lakini pia ingawaje Karume aliuwawa na mwanajeshi cha ajabu ni kuwa uongozi wa nchi haukutwaliwa na jeshi bali alipewa mwanasiasa tu Aboud Jumbe!, haya ni maajabu mengine sasa, hivi huyo Hamid aliyemwua mzee karume alitumwa na wanasiasa? Au? Na kama hajatumwa kwanini baada ya mauaji hayo yaliyofanywa na mwanajeshi tunaambiwa kuwa jeshi lilitaka limpe madaraka kanali Seif Bakari hata hivyo baadaye tunaambiwa liliachana na mpango huo, je nini kiliwasukuma kuacha mpango huo? Na nani aliwakataza kufanya hivyo?
Hatuoni kuwa iwapo jeshi lingempa uongozi kanali Seif Bakari ambaye pia ni mwanajeshi hatuoni kuwa hayo yangekuwa ni mapinduzi ya kijeshi au uasi wa jeshi? Kwanini jeshi limfanye hivo mzee karume? Aliwakosea nini wapiganaji wake hawa?

Kwa maswali mengi kama haya yasiyo na majibu ndiyo inaibuka haja ya kufahamu je nini sababu za mauaji hayo? Nani alikuwa nyuma ya mauaji hayo? Ni wanajeshi au wanasiasa kwa mgongo wa jeshi? Kina nani hao? Na kwanini? Je chuki zilizopelekea mauaji hayo zilikoma au zingalipo hadi leo? Tukiyajua haya itatuweka huru kwa maana ukweli pekee ndio utatuweka huru vinginevyo tunaficha historia yetu kwa hasara yetu wenyewe! Naam ! wakati ni huu watanzania acha sasa tuhoji yasiyohojika!

...Tafakari!


Kitendawili si deni ukishindwa nipe mji,
Kwa wanataaluma kutofautiana kimawazo si kosa bali ni dalili ya jamii iliyo hai,
Nova Kambota Mwanaharakati,
Tanzania, East Africa,

MAONI YA MDAU   
kuna mzee mmoja c jui kama yupo hai ila nilimuuliza kuhusu hilo mika 10 nyuma iliyopita na akanipa historia kwa ufupi
suali no1 karume aliuliwa na nani
jibu karume aliuliwa na aliyekua mtoto wa mfalme humoud bin mohamed
kwa sababu gani alimuua?
katika mapinduzi ya zanzibar wakati karume na washirika wake walifanya mapinduzi kuwadhulumu waarabu na kuwatesa nafsi zao hadi kuwapokonya mali zao na mwisho wakamuua huyu humuod bin mohamed
baada ya hapo wakatangaaza hayo mapinduzi yao mwaka 1964 1967 k.nyerere akamwambia karume tufanye muungano ili wee tupate kukulinda nchi yako ni ndogo watu watakuja kukupindua karume akakubali ila kwa masharti la kwanza muungano uwe kwa muda wa miaka 10 baada ya hapo wanachi waulizwe jee waendelee na muungano au basi ile miaka kumi haikufika karume kavuta.
nani kapanga mauaji?
julius k. nyerere. kabla ya muungano karume wakati yupo katika serikali yake ya zanzibar na yee ndio rais wa kwanza alimpa madaraka mtoto wa humuod bin mohamed alimpa cheo cha ujeshi katika serikali yake alikua ana cheo kikubwa alimpa cheo ili amsahaulishe ule ubaya alio mtendea baba yake baada ya kuunganisha zanzibar na tanganyika hapo nyerere akamwiita mtoto wa humoud bin mohammed akamwambia unajua alie muua baba yako . nyerere akamwambia ni karume basi na wee lazima ukamuue karume kwa vile yeye alikua ni mkubwa katika serikali haikua vigumu kwake alifanya hivyo akamfuata pale makao makuu ya ccm zanzibar na kummiminia risasi mwisho wake na yee akajiua na ndio ukaona toka hapo hadi leo katika serikali ya tanzania hakuna ruhusa ya kupewa ajira ya ujeshi kama wewe ni mwaarabu sio jeshi wala polisi na kama uongo pingeni hilo
nyaraka za muungano mpaka leo hazijuliakni zilipo wapi na kama karume angalikuwepo leo muungano huu ungalisha vunjika zamani
ahsanteni kwa hapo


Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company