


Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka jijini Arusha Oliva Wema akiwaburudisha wakazi wa Iringa mjini mchana leo katika mtaa ya sokoni ukiwa ni mtindo wake wa kuingia sokoni kuuza album zake mbili mwenyewe kama zinavyoonekana nyuma zikinyanyuliwa na kijana wake. Album ya kwanza inaitwa 'Tua Mizigo' na 'Kidomodomo.' Mwimbaji huyo anaelekea jijini Dar es salaam akitokea nchini zambia kupitia Tuduma wilayani Mbozi mkoani Mbeya. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)
