Shangazi ya rais Obama afariki dunia.

Shangazi wa rais Barack Obama Zeituni Onyango wakati wa uhai wake huko Boston.
Shangazi wa rais Obama Zeituni Onyango ambaye kwa wakati fulani alinyimwa hifadhi hapa Marekani lakini akaendelea kuishi kinyume cha sheria kwa miaka kadhaa katika jimbo la Masachussets amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 61.

Wakili wa masuala ya Uhamiaji wa Onyango amesema amefariki katika hospitali moja baada ya kuugua ugonjwa saratani na matatizo ya kupumua . Aliugua tangu mwezi January.
Onyango alihamia Marekani kutoka Kenya mwaka 2000 na alinyimwa hifadhi ya kisiasa na jaji wa Uhamiaji mwaka 2004. Hakuondoka nchini na aliendelea kuishi kwenye nyumba za umma huko Boston. Hali yake ya ukaazi wa Marekani ilitangazwa hadharani siku chache kabla ya Bw.Obama kuchaguliwa rais Novemba 2008.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company