Wanajeshi wanne wa Marekani wauawa Texas


Rais wa Marekani Baracha Obama akiwataka raia wake kuwa watulivu baada ya mwanajeshi kuua wanajeshi wenzake watatu.
REUTERS/Toussaint Kluiters/United Photos   Na RFI
Mwanajeshi wa Marekani, ambaye alikua na “tatizo la akili”, kwa mujibu wa viongozi, ameuwa wanajeshi wenzanke watatu kabla ya kujimalizia maisha, katika kambi ya kijeshi ya Fort Hood, kusini mwa mji wa Texas.
Marekani imekua ikikumbwa na matukio hayo, tukiyo liliyosisimua ni lile liliyotokea mwaka 2009, ambapo watu 13 waliuawa kwa kupigwa risase.

Mwanajeshi huyo alipelekwa nchini Irak mwaka 2011 na alihudumu kwa kipindi cha miezi minne kabla ya kurejeshwa nchini Marekani kutokana na “maradhi ya akili kulingana na ripoti ya daktari aliye mshughulikia”, amesema mkuu wa kmbi hiyo, jenerali Mark Milley.

“Mpaka sasa, hakuna ishara yoyote inaoonyesha kwamba tukio hilo linahusiana na ugaidi, hata kama hali hiyo inaweza ikatokea”, amesema afisa.

Mkuu huyo wa kambi ya jeshi ya Fort Hood amesema, mwanajeshi huyo aliingia katika jengo moja na kuanza kufyatua risase hovyo, kabla ya kuingia ndani ya gari na kufyatua risase kwa mara nyingine akitumia bastola aina ya Smith & Wesson, aliyonunua dukani pembezuni mwa kambi hio.

“Jeshi liliingilia kati kwa kuzingira eneo nzima kulikosikika risase, na kumtafuta mtu huyo aliye kuwa akifyatua risase. Mwanajeshi mmoja alijitahidi kuyatulia risase mtu huyo, lakini kwa bahati mbaya, risase lilimkosa , akamfyatulia risase mwanajeshi huyo aliyejua akimfuatilia”, amesema Mark Milley.

Jeshi linasema mtu aliyetetekeleza mauji hayo ni mwanajeshi na baada ya kufanya hivyo alijiua kwa kujipiga risasi kichwani.

Rais Barrack Obama amesema raia wa Marekani wamevunjika mioyo kutokana na mashambulizi hayo na kusisitiza kuwa uchunguzi unaendelea kubaini ni kwanini mashambulizi hayo yalitokea.

Mwaka 2009 kambi hiyo ya kijeshi ilivamiwa na watu wasiojulikana na kutekeleza mauaji.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company