Na Jackline Charles, Mbeya
KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Frank Domayo amesema amekwishamalizana na Azam FC na kwa vyovyote ataheshimu makubaliano yake na klabu hiyo kwa kuwa yeye ni Mkristo safi.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana mjini hapa, Domayo amesema kwamba amesaini Mkataba wa miaka miwili na Azam FC na amesikia kashikashi alizozipata kiongozi wa klabu hiyo aliyekuja hapa kumsainisha, lakini kwa vyovyote ataheshimu makubaliano.
“Nimesikia, lakini ninavyojua hakuna Mkataba uliochanwa, ila hata kama Mkataba umechanwa, mimi nina nakala yangu, na kwa vyovyote nitaheshimu makubaliano, mimi ni Mkristo safi,”alisema.
Nitaheshimu Mkataba; Frank Domayo kushoto akiwa na meneja wa Azam FC, Jemadari Said kulia baada ya kusaini Mkataba na klabu hiyo juzi mjini hapa
Hata hivyo, Domayo hakutaka kuzungumza zaidi akisema kwa sasa akili yake anaielekeza kwenye mchezo wa Taifa Stars na Malawi Jumapili mjini hapa.
“Hayo yamekwishapita kwa upande wangu, kwa sasa akili yangu naielekeza kwenye mchezo wa Malawi,”alisema.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi jana alisema kwamba amemteua Wakili Wilson Ogunde kuchunguza mlolongo mzima wa tukio la usajili wa Domayo juzi mjini hapa.
Malinzi alisema baada ya kukamilisha uchunguzi wake, Wakili Ogunde ataishauri TFF kuhusu hatua za kisheria na kikanuni za kuchukua. Malinzi ametoa wito kwa wachezaji, klabu na wadau wa mpira wa miguu kufuata kanuni na taratibu katika utendaji wao.
Viongozi wa Azam FC juzi walikwenda kwenye kambi ya Taifa Stars kukamilisha taratibu za usajili na kiungo Frank Domayo, aliyemaliza Mkataba wake Yanga SC.
Baada ya kufanikiwa kumsainisha Mkataba wa miaka miwili, wasimamizi wa kambi waliwaitia Polisi viongozi wa Azam FC ambao hata hivyo baadaye waliachiwa. Lakini inadaiwa fomu za usajili zilichanwa.
Mkristo safi; Frank Domayo amesema ataheshimu makubaliano yake na Azam FC
Azam si klabu ya kwanza kusajili mchezaji katika kambi ya timu ya taifa, kwani vigogo wa soka nchini, Simba na Yanga ndiyo waasisi wa mchezo huo.
Mwaka jana Simba SC walisaini Mkataba mpya na kiungo wao, Amri Kiemba akiwa katika kambi ya Taifa Stars, hoteli ya Tansoma mjini Dar es Salaam.
Yanga SC iliwasajili Domayo kutoa JKT Ruvu, Kevin Yondan kutoka Simba SC wote wakiwa katika kambi ya Taifa Stars Dar es Salaam miaka miwili iliyopita.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago