
Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alisisitiza juu upatikanaji wa masoko ya kudumu kwa mazao yatakayozalishwa katika mpango huo badala ya kuwekeza nguvu katika uzalishaji pekee.

Ndugu Anthony Elanga mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Uyole Jijini Mbeya ambae pia ni Mratibu wa Utafiti wa Zao la Ngano Tanzania akizungumza katika kikao hicho. Amesema mpango huo utahusisha wakulima na vikundi vya wakulima ambao watapatiwa elimu na kuwezeshwa mikopo mbalimbali ya kuendeleza kilimo cha ngano Mkoani Rukwa.

Mkutano ukiwa unaendelea.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)

