Msimamo huo ulielezwa na viongozi hao kwa nyakati tofauti katika mkutano wa hadhara uliofurika mashabiki kwenye Viwanja vya Mwembetogwa katika Manispaa ya Iringa, mkoani Iringa jana.
Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba alisema wajumbe wa Ukawa wameamua kujitoa bungeni kutokana na kauli mbalimbali za CCM ambayo alidai kuwa waliibeza na kuidhalilisha Tume ya Warioba.



Wakazi wa Manispaa ya Iringa wakirudi makwao baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara jana jioni

