Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) imelaani hatua ya baraza la mawaziri la utawala haramu wa Israel ya kuidhinisha sheria inayopiga marufuku kuachiliwa huru wafungwa wa Palestina na kusema hatua hiyo ni hatari kwa mustakabali wa amani ya Mashariki ya Kati. Naibu Katibu Mkuu wa Arab League anayehusika na masuala ya Palestina na ardhi za Waarabu zinazokaliwa kwa mabavu, Mohammad Swabih, amesema kuwa hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuzuia kuachiliwa huru wafungwa wa Kipalestina inaonyesha jinsi utawala huo ghasibu ilivyokubuhu katika unyama na dhulma. Swabih ameongeza kuwa, Israel kwa kuchukua uamuzi huo imeonyesha ulimwengu kwamba haina nia ya kuruhusu kuweko taifa huru la Palestina kwani hatua hiyo imefunga kabisa mlango wa mazungumzo kati ya PLO na Tel Aviv.
Jana Jumapili utawala wa Kizayuni uliidhinisha sheria inayopiga marufuku kuachiwa huru wafungwa wa Kipalestina. Kwa mujibu wa sheria hiyo, hata rais wa utawala huo bandia hana mamlaka ya kuwasamehe wafungwa au kuwapunguzia vifungo vyao bila idhini ya mahakama.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago