MBUNGE FILIKUNJOMBE ATOA MSAADA

Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akizungumza na waumini wa kanisa la RC Madunda mara baada ya kusaidia kanisa hilo kiasi cha Tsh milioni 15 za ukarabati wa kanisa na vinanda viwili vya kwaya kanisani hapo


Viongozi wa kanisa hilo wakimshangilia mbunge huyo kwa msaada wake




Waumini wa kanisa hilo wakifurahia misaada ya mbunge wao



katibu mwenyezi wa wilaya ya Ludewa Filix Haule (kushoto ) na mmoja kati ya madereva wa mbunge Filikunjombe Bw Andondile wakisogeza vinanda viwili vya kisasa kwa mbunge Filikunjombe



Mbunge Filikunjombe kulia akikabidhi msaada wa vinanda kwa viongozi wa kwaya katika kanisa la RC Madunda



Mbunge Filikunjombe kulia akizungumza jambo na paroko msaidizi wa Madunda baada ya kutoa mchango wake wa Tsh milioni 15 kwa ajili ya kukarabati kanisa mchango ambae kiusalama aliahidi kuuweka katika akaunti ya jimbo

Mbuge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe amechangia kiasi cha Tshmilioni 15 kwa ajili ya ukarabatiwa kanisa la Roman Katorikiparokia ya Madunda wilayani Ludewa pamoja na kusaidia vinanda
viwili kwa kwaya mbili kanisani hapo.Akikabidhimsaada huo leo mara baada ya ibada ya jumapili mbungeFilikunjombe alisema kuwa amefika kanisani hapo baada ya kuombakinada na kwaya ya kanisa hilo na hivyo kutokana na kuwepo kwakwaya mbili amelazimika kutoa msaada wa vinanda kwa kwaya zotepamoja na kusaidia kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya ukarabati wa

kanisa hilo.Kwanialisema kuwa kanisa hilo ni mmoja kati ya makanisa makongweyaliyojengwa miaka ya 1980 katika wilaya hiyo ya Ludewa na kuwakanisa hilo ndilo kanisa la tatu kujengwa kwa wilaya ya Ludewahivyo linahitaji kufanyiwa ukarabati mkubwa ili kuendeleakuwafanya waumini wa kanisa hilo kupata eneo la kuabudia.Filikunjombealiwataka waamuni hao na waumini wa madhehebu mengine katikawilaya ya Ludewa kuendelea kumwombea afya njema ili kupata nguvuya kuwaletea maendeleo kama ambavyo ameendelea kufanya katikawilaya hiyo kama njia ya kuwashukuru wananchi wake kwakumwamini katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kwa kumchagua kuwambunge wa jimbo hilo la Ludewa ."Imani ambayo wenzangu wananchi wa Ludewa mlioionyesha mwaka 2010 katikauchaguzi mkuu kwa kunichagua kuwa mbunge kamwe sitaachakuwakumbuka wananchi wangu wa Ludewa kila ninapokuwa bungenimawazo yangu kurejesha ahsante yangu kwangu na kuona wilaya yetuya Ludewa inaendelea kupiga hatua"Piambunge huyo alisema kwa sasa mkakati wake na wa serikali yaRais Dr Jakaya Kikwete ni kuona ujenzi wa barabara ya lami kutoka Njombe hadi Ludewa inajengwa na tayari wakandarasi wakuanza ujenzi huo wamekwisha patikana ndani ya miaka hii miwilibararabara hiyo itakuwa imejengwa na ujenzi wake utafanyika kwaawamu tofauti.Hatahivyo alisema kuwa akiwa mbunge wa jimbo hilo kamwe hatakubalikuona wana Ludewa anawapelekea maendeleo kwa upendeleo na kuwalazima pande zote ikiwemo la milimani , mwambao wote wananufaika namatonda yake kwa kuwa na maendeleo wote.Kwa upande wake katibu wa itikadi na uenezi wa mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya akimpongeza mbunge huyo kwa kuendelea kusukuma mbele maendeleo ya jimbo hilo ,alisema kuwa kazi zinazofanywa na mbunge huyo zimekipatia heshima chama cha mapinduzi (CCM) na kuwa utendaji mzuri wa kazi wa mbunge huyo ndio ambao umeitangaza wilaya ya Ludewa .

VICTOR SIMON
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company