Meneja wa Vipindi wa East Africa Radio, Nasa Kingu (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu kampeni ya kuhamasisha vijana inayojulikana kama `Zamu yako kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa 2015.' Kushoto ni Mtangazaji wa redio hiyo, Abdallah Ambua na kulia ni Meneja wa Masoko wa EATV, Alex Galinoma.PICHA: SELEMANI MPOCHI
Vijana nchini wameandaliwa kampeni ya kuwahamasisha na kuwaelimisha kwa ajili ya kushiriki katika upigaji kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa na uchaguzi mkuu mwaka huu.
Kura ya maoni ya kukubali au kuikataa Katiba inayopendekezwa itafanyika Aprili 30, mwaka huu na uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika Jumapili ya mwisho ya Oktoba, mwaka huu.
Kampeni hiyo itwayo `Zamu yako 2015' imeandaliwa na Kituo cha Runinga cha EATV na Redio ili kuwaelimisha vijana kujiandikisha katika daftari la wapigakura, kupigia kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa na uchaguzi mkuu wa kuwachagua madiwani, wabunge na rais.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa vipindi vya EATV na Redio, Nasser Kingu, alisema kuwa katika kuhakikisha lengo lao linatimia, vituo hivyo vitatumia vipindi na matanagazo mbalimbali kwa kuwahusisha wadau ambao watatoa elimu kuhusu umuhimu wa vijana kushiriki katika upigaji kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa na uchaguzi mkuu.
“Kupitia vipindi vyetu na matangazo, tunaamini kwa kiasi kikubwa itasaidia vijana kufahamu mambo mazuri yaliyomo katika Katiba inayopendekezwa na kupiga kura kuchagua viongozi wanaofaa kwa maisha yao na watoto wao,” alisema Kingu.
Kingu alisema wameamua kufanya kampeni hiyo kwa kuwa imebainika kuwa katika taifa lolote duniani, vijana ndilo kundi kubwa linaloweza kuchochea mabadiliko ya haraka.
Aidha, alisema takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, zinaonyesha kuwa vijana wenye umri wa miaka 18 kwenda juu, wana sifa ya kushiriki kupiga kura wakati Watanzania takriban 22,424,136 wakitarajiwa kushiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Alisema kati ya idadi hiyo, vijana kuanzia miaka 18 hadi 40 ambao ni asilimia 68.20 ya Watanzania wenye sifa ya kupiga kura.
Aliongeza kuwa hii si mara ya kwanza kwa EATV kuandaa kampeni hiyo kwani mwaka 2010 kituo hicho kiliandaa kampeni iliyojulikana kama ‘Kijana acha kulalamika tumia kura yako kuleta mabadiliko’, ambayo alisema hata hivyo, haikufanikiwa kutokana na kuanza kuhamasisha badala kutoa elimu kwanza.
CHANZO: NIPASHE
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago