KOVA APIGA MARUFUKU MAANDAMANO YA VIJANA WA CUF

Kamishna Kova akizungumza na wanahabari (hawapo pichani)


Wanahabari wakimsikiliza Kamishna Kova (hayupo pichani)

KAMISHNA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar e s Salaam, Suleiman Kova jana ametoa tamko mbele ya wanahabari juu ya maandamano ya vijana wa Chama cha Wananchi CUF (JUVICUF) yaliyokuwa yamepangwa kufanyika hapo kesho.

Kamanda Kova amewataka vijana wa CUF kutoandamana kesho na kama wataandamana jeshi hilo halitakuwa tayari kuona maandamano hayo yakifanyika .

Alisema kuwa maandamano hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika kesho Februari 13 mwaka huu kutoka Buguruni, Shule ya Uhuru, Mnazi Mmoja, Mtaa wa Ohio hadi Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kisha Wizara ya Mambo ya Ndani ,kwa dhumuni la kuitaka Tume ya Taifa ya Uchanguzi (NEC) iongeze siku za uandikishwaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kutoka siku saba hadi siku 14, pamoja na kulaani ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na jeshi la polisi nchini.

Kova ametaja sababu za kuzuia maandamano hayo kuwa siku waliyoomba ni siku ya kazi, ambapo maandamano hayo yakifanyika yatasumbua mfumo mzima wa shughuli za jiji zima, kibiashara, huduma za afya, walemavu, watoto na n.k.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Vijana wa Chama cha CUF, Hamidu Bobali akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Anthony Siame
(Habari/Picha: Gabriel Ng’osha/GPL)
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company