Libya yaomba kuondolewa vikwazo

Afisa wa Libya katika kikao cha kimataifa
Serikali ya Libya inayotambuliwa kimataifa imeliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuiondolea nchi hiyo vikwazo vya silaha ili kukabiliana na kuzorota kwa hali ya usalama nchini humo.

Akihutubia kikao cha dharura cha baraza hilo, waziri wa mambo ya nje wa Libya,Mohammed al-Dairi amesema hatua hiyo itaisaidia serikali ya Libya kujenga jeshi lake, ili kuwatokomeza Islamic State na makundi mengine ya wapiganaji.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Libya aliungwa mkono na waziri wa mambo ya nje wa Misri Sameh Shoukry, ambaye amesema jumuia ya kimataifa inatakiwa kuisaidia serikali ya Libya ili kuonyesha mamlaka yake nchini humo.

Mapema wiki hii, ilithibitika kuwa wapiganaji wa Islamic State nchini Libya waliwakata vichwa mateka kutoka Misri.
CHANZO BBC SWAHILI
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company