Ukraine yaomba msaada wa ulinzi

Rais Petro Poroshenko wa Ukraine akizungumza na vyombo vya habari katika uwanja wa Kiev kabla ya kusafiri kwenda Donetsk

Rais wa Ukraine Petro Poroshenko, amevitaka vikosi vya umoja wa mataifa vya kulinda amani kupelekwa mashariki mwa nchi hiyo ili kuhakikisha zoezi la kusitishwa kwa mapigano linafanikiwa.

Ametoa wito huo katika mkutano maalum wa dharura wa baraza la usalama, baada ya vikosi vya Ukraine kujitoa katika mji wa mashariki wa Debaltseve kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na waasi wanaoungwa mkono na Urusi. Pande zote mbili zimekuwa zikilaumiana kwa kukiuka makubaliano ya kusitishwa kwa mapigano yaliyofikiwa wiki iliyopita.

Kwa upande wake, serikali ya Marekani imesema Urusi na kundi la waasi linaloliunga mkono wameshindwa kutimiza makubaliano yaliyosainiwa wiki iliyopita na viongozi wa Ujerumani, Ukraine, Ufaransa na Urusi.

Viongozi hao wanne walipanga kujadiliana kuhusu mustakbali wa eneo hilo jana usiku.

Awali msemaji wa kansela wa Ujerumani Angela Merkel, amesema makubaliano hayo yanapitia wakati mgumu.
CHANZO BBC SWAHILI
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company