Baada ya kujificha msituni kwa miezi kadhaa, kuwatoroka wapiganaji wa al-Shabaab, al-Amriki alitangaza kujitenga kwake na al-Shabaab na al-Qaeda katika mahojiano yaliyofanywa kwa njia ya simu kupitia Sauti ya Amerika (VOA) tarehe 3 Septemba.
Kisha, tarehe 5 Septemba -- wiki moja kamili kabla ya kuripoti kusambaa kwamba al-Amriki aliuawa na wanaume wenye silaha wa al-Shabaab-- Rasmi News ilitoa video isiyokuwa na tarehe ikionyesha mwanajihadi huyo akizungumza kwa Kisomali.
Katika mawasiliano yote mawili, al-Amriki, ambaye pia anajulikana kama Omar Hammami, alilenga kwenye upinzani wake mkali kwa uongozi wa Godane.
"Sababu ya tatizo hilo kimsingi ni kwamba [Godane] aliacha kanuni za dini yetu na anajaribu kubadilisha l-Shabaab kuwa asasi ambayo inakandamiza kila Muislamu katika jitihada za kujifanya ndiye Siad Barre anayefuatia wa Somalia," al-Amriki aliiambia VOA wakati akihojiwa kuhusu tofauti yake na Godane, ambaye pia anajulikana kama Abu Zubayr.
Godane anataka kuwa "kiongozi wa Somalia ama awe anaongoza kwa sharia au kwa sheria nyingine zozote," al-Amriki alisema. "Kimsingi amepoteza kanuni kuu ambayo ndilyo iliyofanya jihadi ianzishwe."
Wakati alipoulizwa kwa nini Godane aliendelea na kampeni yake ya kumuua al-Amriki na wafuasi wake, al-Amriki alijibu, "kwa sababu ninajua vya kutosha kuhusu asasi yake kujua kwamba hakufuata kanuni za Kiislamu".
www.hakileo.blogspot.com
"Na hakutaka ijitokeze kwa umma, na kisha inaweza kufika mahali kama vile Yemen au Iraq … na hata al-Qaeda -- watu anaojaribu kuwabelembleza wakati akijaribu kuwa kama wao," alisema.
"[Pia] mimi ni mmoja wa watu wachache nchini Somalia ambaye nilisimama dhidi ya al-Shabaab kuwalipua raia wasio na hatia, hiyo ndiyo moja ya sababu ya Abu Zubayr angependa nife," al-Amriki alisema.
"Kwa kuhitimisha, unaweza kumwita mdhibiti wa kweli. Anajali tu wale walio katika nafasi yake na madaraka juu ya yeyote anayejiita Mwislamu," alisema. "Na kama sharia inakuja kwa wale wenye malengo kama yake, anaipeleka sheria nje ya mkondo wake."
Wakati mhoji alipomuuliza al-Amriki kuhusu nini alichokifanya kuhusu Godane, alijibu, "Kitu pekee niinachoweza kufanya ni kuweka wazi njia zake za uonevu."
"Abu Zubayr anazuia Qur'an na Sunnah," alisema.
Godane afukuzwa kama amiri wa al-Shabaab
Katika video isiyo na tarehe, al-Amriki alielezea kwa kina kuhusu Godane alivyokataa kuwasilikiza viongozi wengine wa juu wa al-Shabaab wakati kikundi cha wanamgambo kilipopoteza haraka maeneo kwa vikosi vya Somalia na vya kimataifa. Wakati fulani, maneno katika video hayaeleweki kwa sababu ya al-Amriki kutoelewa vizuri lugha ya Kisomali.
Al-Amriki anaeleza jinsi Baraza la Shura la al-Shabaab na idadi ya viongozi wa juu wa kundi la wanamgambo -- akiwemo Ibrahim al-Afghani, Sheikh Mukhtar Robow Ali na Fuad Mohamed Khalaf -- walivyojaribu kusuluhisha na Godane katika jitihada za kuboresha sifa ya jihad huko Somalia.
Alisema Zubayr al-Muhajir, mkuu wa baraza la usuluhishi, alipewa mamlaka ya kumfukuza Godane kama ingejulikana kwamba kiongozi huyo wa al-Shabaab ameshindwa kusuluhisha tofauti za kikundi.
Godane hakusubiri baraza lifanye uamuzi, lakini badala yake alimteua Sheikh Maalim Burhan kumchagua amiri. Burhan, ambaye alikuwa kiongozi wa Baraza la Shura, aliamua kwamba wajumbe wa baraza kwa pamoja wanapaswa kufanya uamuzi.
"Abu Zubayr alikataa kufuata maagizo ya baraza, lakini alikubali kujiuzulu kutoka katika uongozi wa amiri baada ya miezi kadhaa," al-Amriki alisema.
Lakini Godane kamwe hakuachia nafasi yake.
Muda mfupi baadaye, Godane alivunja baraza na kikosi cha Amniyat cha al-Shabaab, ambacho kinamtii Godane, aliwatishia wajumbe wa baraza kwa kuuawa au kufungwa, kwa mujibu wa al-Amriki.
Kufichuka kwa Al-Amriki kulithibitisha na kuongezea kile kilichokuwa kimesemwa katika barua ya wazi ya Zubayr al-Muhajir iliyowekwa katika tovuti ya wanajihadi tarehe 20 Aprili na barua ya Ibrahim al-Afghani iliyotolewa mapema mwezi huo.
Akitimiza ahadi yake: Godane awaua waasi
Al-Shabaab imekubali wazi kwamba vikosi vyake viliwaua viongozi wawili muhimu waliopinga uongozi wa Godane -- Ibrahim al-Afghani na Sheikh Maalim Burhan -- kufuatia mapigano huko Barawe mwezi Juni kati ya vikundi vinavyopingana vya al-Shabaab.
Lakini wakati al-Shabaab walipojaribu kuonesha vifo vyao vilitokana na kupigwa risasi, vyanzo vingi vilidai wanaume hao wawili walipelekwa msituni nje ya Barawe na kuuawa bila ya kushtakiwa.
Katika mahojiano na VOA, al-Amriki alithibitisha kuuawa kwao.
Vifo vya al-Afghani na Burhan "havihusiani na Uislamu, na vinahusika tu na kuzuia nafasi ya Abu Zubayr ili kumbakiza kama kiongozi wa ardhi yoyote ambayo bado iko chini ya udhibiti wake", alisema, akiongeza kwamba miili yao ilizikwa katika eneo lisilojulikana ili kuficha kile walichokifanya wanaomtii Godane.
Kuhusiana na hadhi ya kiongozi mwandamizi wa al-Shabaab Mukhtar Robow Ali, al-Amriki alisema "pia yuko msituni kwa sasa na yuko katika tishio la moja kwa moja la kushambuliwa na al-Shabaab kila siku kwa sababu anapingana na mauaji ya raia."
"Lakini kwa sasa hadhamirii kufanya chochote kuhusu [Godane] isipokuwa kuendelea kukaa msituni," al-Amriki alisema, akiongeza kwamba Robow alikuwa anahofia kwamba al-Shabaab walikuwa wanafuatilia simu yake.
Al-Amriki amekufa kweli?
Wakati ushahidi unaonesha kushawishi vya kutosha kuashiria kwamba kwa kweli al-Amriki aliuliwa na wapiganaji wa al-Shabaab, hii sio mara ya kwanza kifo chake kimedaiwa kutokea.
Kifo cha al-Amriki kimeripotiwa mara kadhaa ndani ya miaka miwili iliyopita. Hapo mwezi wa Machi 2012, al-Amriki alisema alihofia maisha yake kutoka kwa viongozi wa al-Shabaab kutokana na tofauti za kiitikadi, na vyombo vya habari viliripoti kuwa aliuawa mwezi wa Aprili.
Ripoti hizi baadaye zilikanushwa na al-Amriki kujitokeza katika video kadhaa za mtandaoni na alikuwa akitumia sana tovuti za kijamii hadi mwezi wa Mei 2013, wakati taarifa za kifo chake mikononi mwa al-Shabaab ziliposambazwa tena.
Lakini al-Amriki akajichomoza tena katika majadiliano na Sauti ya Amerika mapema mwezi huu na kurejea kwa muda mchache katika Twitter.
Uvumi wa mwisho juu ya kifo cha al-Amriki unaonekana kuwa wa kweli, hata hivyo, kwa sababu taarifa za awali ziliwanukuu baadhi ya watu ambao walimwelewa vyema al-Amriki, na katika akaunti yake ya Twitter pia kulitumwa ujumbe tarehe 15 Septemba: "Tunathibitisha ushahidi wa Omar Hammami asubuhi ya Alhamisi tarehe 12 2013. Familia ya Shafik tafadhali pokeeni rambirambi zetu."
Mara nyengine katika miaka miwili iliyopita, ilionekana kwamba watu wengi walikuwa wanatumia akaunti ya Twitter ya al-Amriki kwa sababu mtindo na kumudu kwao Kiingereza kulitofautiana miongoni mwa machapisho yao. Ukweli huu unaunga mkono mawazo kwamba mmoja wa wafuasi wake alituma ujumbe huo wa mwisho kwenye Twitter.
Hatimaye, miongoni mwa maneno ya mwisho ya al-Amriki -- kudai kwamba alikuwa amekufa kikweli kweli -- yalikuja kwa kukubali kwamba, mbali na kukata mahusiano na al-Shabaab na al-Qaeda, mwanajihadi huyo mwenye umri wa miaka 29 alikuwa amekata uhusiano na Marekani moja kwa moja na kamwe asingerejea tena alikozaliwa.
Wakati mtu wa VOA aliyekuwa anamhoji al-Amriki alipomuuliza kuhusu kutembelea familia yake huko Marekani, yeye alijibu, "Hilo haliwezekani kabisa kabisa isipokuwa ikiwa kwenye mfuko wa kubebea miili."