Michuano ya ligi ya mabingwa wa Ulaya imeendelea leo tena katika hatua ya 16 bora ya michuano ambapo mabingwa wa England, Manchester City waliikaribisha FC Barcelona katika dimba la Etihad katika mchezo wa raundi ya kwanza ya hatua hiyo ya mtoano wa michuano hiyo.
Barca ambao waliitoa City katika michuano hii msimu uliopita, wamefanikiwa kuingiza mguu mmoja ndani kwenye hatua ya robo fainali baada ya kupata ushindi wa 2-1.
Magoli ya FC Barcelona yalifungwa na Luis Suarez katika dakika ya 16 na 30 ya mchezo.
Sergio Aguero aliifungia City goli la kufutia machozi katika dakika ya 69.
Mechi hiyo itarudiwa wiki mbili zijazo katika dimba la Camp Nou ndani ya Jiji la Barcelona.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago