Watu waliojeruhiwa na bomu huko Nigeria Nuwamba 29, 2014.
Mlipua mabomu wa kike aliyejitoa mhanga nchini Nigeria ameuwa watu wasiopungua 10 na kujeruhi zaidi ya 30 Jumapili wakati alipojilipua katika kituo cha basi kilichojaa watu.
Mlipuko huo ulitokea katika mji wa kaskazini mashariki wa Darmaturu katika jimbo la Yobe huku mashahidi na maafisa wakisema msichana mmoja alifanikiwa kuwapita maafisa usalama katika kituo cha ukaguzi kabla ya kujilipua.
Shirika la habari la Ufaransa lilisema kundi la watu wenye hasira lilizuia wafanyakazi wa uokozi kuchukua mabaki ya mlipua mabomu huyo wa kujitoa mhanga na kuamua kuchoma mabaki yake .
Mashahidi wanasema waathirika wengi wa shambulizi hilo walikuwa ni watoto waliokuwa wakiuza bidhaa za rejareja kwenye kituo hicho cha basi wakijitafutia riziki.
CHANZO VOASWAHILI
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago