|
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu |
Nyaraka za siri zilizochapishwa na gazeti la Guardian la London ambazo waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alizihusisha na mpango wa nyuklia wa Iran 2012 imebainika kuwa madai hayo hayakuungwa mkono na idara za usalama za Israel. Tuhuma hizo za Israel dhidi ya Iran zilitolewa na Netanyahu mwaka 2012. Moja ya taarifa hizo zilizovuja kupitia jalada hilo la Mossad lilionyesha kuwa Iran haikuwa na mpango wa uzalishaji Uranium kwa matumizi ya kawaida bali kutengenezea mabomu. Afisa mwandamizi wa Irael ameeleza kuwa jalada hilo la Mossad lililobeba kashfa hiyo kamwe halihusiani na kubeza madai ya Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuhusia na Iran na mpango wake wa Nyuklia. Chapisho hilo linadaiwa kuwa ni moja kati ya mamia ya machapisho ya siri yanayobeba taarifa za uchunguzi zilizofanywa na Al Jazeera kwa kushirikiana na gazeti la Guardian.