Michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, hatua ya kumi na sita bora, iliendelea Jumatano usiku kwa kuzikutanisha timu za FC Basel ya Uswisi na FC Porto ya Ureno katika mchezo ambao FC Basel ndio waliokuwa wenyeji na mchezo wa pili ukiwa kati ya wenyeji Schalke 04 ya Ujerumani dhidi ya mabingwa watetezi Real Madrid ya Hispania.
Tuanze na mchezo wa FC Basel dhidi ya FC Porto. Mpambano huo ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1. Wenyeji FC Basel ndio waliokuwa wa kwanza kujipatia goli katika dakika ya 11 likifungwa na Gonzalez ambalo lilidumu hadi kipindi cha pili, FC Porto waliposawazisha katika dakika ya 75 kwa mkwaju wa penalti iliyofungwa na Danilo baada ya mchezaji wa FC Basel Samuel Walter kuunawa.
Katika mchezo huo ambao ulitawaliwa kwa kiasi kikubwa na wageni, FC Porto wakimiliki kwa asilimia 63% huku wenyeji wakiwa na asilimia 37% ulimalizika kwa mwamuzi wa mchezo huo Clattenburg kuwaonya wachezaji tisa kwa kadi za njano, watano wakiwa ni wa FC Basel na wanne kutoka FC Porto.
Kocha Carlo Ancelotti wa Real Madrid akishangilia goli na wachezaji wakeMchezo mwingine ulikuwa katika dimba la wenyeji Schalke 04 dhidi ya Real Madrid, ambapo Real Madrid waliibuka kwa ushindi wa mabao 2-0 yakifungwa na Cristiano Ronaldo na Marcelo. Real Madrid walipata goli lao la kuongoza dakika ya 26 likifungwa na Ronaldo na goli la pili lilifungwa na Marcelo dakika ya 79 ya mchezo.
Ronaldo amekuwa na magoli 58 katika michezo 58 ya ligi ya mabingwa. Mpaka sasa Real Madrid inaongoza katika hatua hii ya kumi na sita bora kwa michezo ambayo tayari imechezwa na timu nane tangu itimue vumbi hapo juzi Jumanne usiku.
Real Madrid ilitawala mchezo huo kwa asilimia 61% huku Schalke wakimiliki kwa asilimia 39%. Mwamuzi wa mchezo huo Martin Atkinson aliweza kuwazawadia kadi za njano wachezaji wanne, watatu kutoka Schalke na mmoja ni wa Real Madrid.
Michezo inayokuja itachezwa tarehe 24 na 25 mwezi huu kwa Juventus ya Italia kuialika Bor Dortmund ya Ujerumani na Man City ya England ikiwakaribisha Barcelona ya Hispania. Na tarehe 25 itakuwa patashika nguo kuchanika kwa Arsenal ya England kucheza na Monaco ya Ufaransa huku Bayer Levkusern ikipepetana na Atletico Madrid ya Hispania.CHANZO:BBC
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago