Waziri wa Fedha wa Ugiriki Yanis Varoufakis
Serikali ya Ugiriki imeleezea imani yake kwamba mkataba kuhusu madeni yake, utafikiwa ndani ya saa arobaini na nane, licha ya kupinga muda wa mwisho uliowekwa na nchi za Ulaya zinazotumia sarafu ya euro.
Mkutano wa mawaziri kutoka nchi za Ulaya zinazotumia sarafu ya euro waliokutana mjini Brussels, Ubalegiji ulivunjika mapema kuliko ulivyotarajiwa wakati serikali ya Ugiriki kutupilia mbali fursa iliyotolewa kwa nchi hiyo hadi Ijumaa kuhusu mpango wa nchi hiyo kudhaminiwa, au kuona mipango ikiisha kufikia mwishoni mwa mwezi huu.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya serikali ya Ugiriki vinasema pendekezo la nchi za ulaya ni "upuuzi" na "halikubaliki".
Lakini waziri wa fedha wa Ugiriki, Yanis Varoufakis, amesema Ulaya itafanya "ulaghai uliozoeleka" kwa kutumia mkataba usio na ufumbuzi wa hali iliyopo.
Serikali ya Ugiriki inataka kumaliza masharti iliyowekewa katika deni lake la euro bilioni mia mbili na arobaini. Lakini bila ya fedha za nyongeza kufikia mwishoni mwa mwezi, inaweza kukosa fedha.)
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago