Rais Joseph Kabila wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Upinzani nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umepokea kwa furaha hatua ya tume ya uchaguzi ya nchi hiyo kutangaza tarehe ya uchaguzi.
Hapo jana Tume ya Uchaguzi nchini humo ilitangaza uchaguzi mkuu wa rais na wabunge utafanyika Novemba 27 mwaka 2016 na kutanguliwa na uchaguzi wa serikali za mitaa baadae mwaka huu.
Kutangazwa kwa tarehe hiyo ya uchaguzi mkuu kunakuja wiki chache baada ya ghasia zilizotokea katika miji kadhaa nchini humo kupinga sheria ya uchuguzi mbayo ingesogeza mbele tarehe uchaguzi.
Upinzani na wanaharakati walipinga sherika hiyo kwa madai ilikuwa ni njama za Rais Joseph kabila kuchelewesha uchaguzi huo ili aendelee kutawala.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago