ABIRIA DHIBITINI MADEREVA-RC

Na Hastin Liumba, Nzega
KUFUATIA ajali iliyohusisha magari manne katika Kijiji cha Undomo, Kata ya Uchama wilayani Nzega mkoani Tabora na kusababisha vifo vya watu sita papo hapo na majeruhi tisa.

Abiria wametakiwa kuwadhibiti madereva wanaokwenda mwendo kasi pindi wanapo safari.

Akizungumza viwanja vya polisi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Tabora Ludovick Mwananzila, mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Selamani Kumchaya alisema ajali nyingi zimekuwa zikitokea kwa uzembe wa madereva kutozingatia sheria Barabarani.

Alisema jukumu hili linapaswa kusimamiwa na abiria pindi wanaposafiri kwa kutafuta njia za kudhibiti madereva waendao mwendo kasi ikiwa na kutoa taarifa pahala husika.

Alisema ajali hiyo iliyotokea March 23 mwaka huu haijawahi kutokea wilayani hapo na kuongeza watu wamepoteza maisha ikiwa na watumishi wanne wa halmashauri ya wilaya ya Nzega.

Mkuu wa wilaya ya Nzega Jackline Liana alisema wananchi wanapaswa kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki kigumu na kuongeza kuwataka madereva wafuate sheria za barabarani.

Alisema gari la halmashauri lenye namba za usajiri SM 4905 lilikosa mwelekeo na kugongana na magari matatu likiwepo gari namba T 831 DDK aina ya Centa gari nyingine RAV4 T654 ASQ kisha kukutana uso kwa uso na bas la Super Shem T 874 CWE likitokea Dar es salaam na kusababisha vifo vya watu sita na majeruhi tisa.

Aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni Dereva wa gari la halmashauri Charles Sanga ,Emmanuel Kasenyi Mhasibu halmashauri,Peter Steven Bwana Afya wilaya, Robert Kisabho mtumishi, Yasinta Alex mkazi wa Isunga na Matukuta Malikita na kuongeza kuwa majeruhi wengine wanaendelea vizuri.

Mamia ya wananchi wa Nzega walijitokeza kuaga marehemu hao licha kuwatoonekana sura zao kutokana na miili hiyo kuelezwa kuwa imeathirika sehemu kubwa ya majeraha
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company