Hussein Rajabu atowa wito wa ushirikiano na Rais Nkurunziza wa Burundi

Hussein Rajabu mwenyekiti wa chama cha CNDD-FDD, akihutubia mkutano wa hadhara

Mwenyekiti wa zamani wa chama tawala cha Burundi cha CNDD-FDD, Hussein Rajabu ametowa wito kwa rais Pierre Nkurunziza, kuwaachia huru wafungwa wote wa kisiasa na kumshirikisha kila mtu katika utaratibu wa uchaguzi mkuu ujao kwa maslahi ya Burundi.

Akizungumza kwa mara ya kwanza na Sauti ya Amerika tangu kukimbia kutoka jela, akiwa uhamishoni, Bw Rajabu anasema yuko katika hali ya usalama na afya nzuri na yungali na nia ya kuleta mabadiliko na mageuzi ya kisiasa nchini mwake kwa ushirikiano na wote na kwa faida ya Warundi wote.

Akizungungumzia juu ya namna alivyotoroka hakufafanua moja kwa moja nani walyemsaidia ispokua kusema "kwa hakika mimi sikukimbia kwa sababu nimetoka kwa heshima kabisa. Ndugu zangu ambao tulihangaika pamoja msituni waliweza kuchukua hatua wakishirikiana nami kufanya kila liwezekanalo ili niweze kuwa huru"

Mwenyekiti huyo wa zamani wa chama cha CNDD-FDD amesema sababu ya kusubiri hadi hivi sasa kuondoka ni kutaka Warundi na Jumuia ya Kimataifa kufahamu matatizo halisi ya Burundi. Mambo hayo yamedhihirika wazi anasema, nayo ni kutoheshimu demokrasia, kutoheshimu mali ya umaa na mambo yote walokubaliana ili kuwawezesha "Warundi waweze kupumua baada ya utawala wa kimabavu."
CHANZO VOA SWAHILI
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company