Waziri Mkuu wa Israel ameyashutu vikali mataifa yenye nguvu ya nchi za magharibi kuhusu majadiliano na Iran juu ya mpango wa nyuklia, lakini Rais Obama amesema hotuba ya Benjamin Netanyahu kwa bunge la Congress la Marekani haikuwa na njia mbadala ya kushughulikia tatizo hilo.
Bwana Obama amesema njia mbadala pekee ambayo waziri mkuu Netanyahu ametoa ni "hakuna mkataba".
Amesema katika hali hiyo, Iran haraka itaanza kuendelea na mpango wake wa nyuklia ikiendeleza mpango wa nyuklia bila sisi kujua wanachokifanya na bila kizuizi na hoja yake ya msingi ni kwamba iwapo tunazidisha vikwazo dhidi ya Iran, haitataka kuendelea na mpango huo.
"Tumekuwa na ushahidi kutoka miongo iliyopita kwamba vikwazo vipekee havitoshi kuizuia Iran kuendelea na na mpango wake wa nyuklia na kwamba hoja hiyo haina mashiko kwamba vikwazo vikiondolewa haitakuwa na hali ya kuogopa njia inayopitia sasa," amesema Obama.
Kwa upande wake waziri mkuu huyo wa Israel, Bwana Netanyahu amekuwa akipinga vikali hali ya kuwepo mazungumzo na Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia akisema kuwa mpango wa nyuklia wa Iran ni "hatari kwa usalama wa taifa la Israel na watu wake".
CHANZO BBC SWAHILI