Ona Jinsi Balozi wa Marekani alivyoshambuliwa

Balozi Mark Lippet akiwa na majeraha baada ya shambulizi.

Balozi wa Marekani nchini Korea Kusini ameshambuliwa kwa kisu usoni na pia katika kifundo cha mkono wake na mshambuliaji aliyekuwa akibwata kuhusiana na suala la kugawanywa kwa kipande cha ardhi ya jumuiya yao.

Mara tu baada ya shambulio hilo Rais wa Marekani Barack Obama amemtakia uponaji wa haraka msaidizi wake wa zamani Mark Lippert akimuombea uponaji wa haraka baada tu ya shambulio lililofanywa wakati wa hotuba ya asubuhi.

Balozi huyo mwenye umri wa miaka 42 alikimbizwa hospitalini ambako alifanyiwa upasuaji wa zaidi ya saa mbili ingawa madaktari wamethibitisha majeraha yake hayatarishi maisha yake.

Jeraha lake limekadiriwa kuwa na sentimeta kumi na moja upande wa kushoto na ameshonwa nyuzi themanini kwenye mkono uliokatwa shambulio lililosababisha baadhi ya mishipa kushindwa kufanya kazi.Msemaji wa Ikulu ya Marekani amelaani kitendo hicho kwa nguvu zote .

Baada ya shambulio hilo maofisa wa polisi walionekana wakimrukia na kumdhibiti mshambuliaji aliyekuwa na kisu chenye urefu wa inchi kumi.

Polisi wamemtambua mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 55 aitwaye Kim Ki-Jong, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya shambulio kam hilo kwa kumshambulia balozi wa Japan nchini Seoul mnamo mwaka 2010.

Mkuu wa polisi Yoon Myung na amesema kwamba wanamshikilia mtuhumiwa huyo na wanachunguza sababu ya shambulio hilo na masuala mengine kumhusu .Askari wakiwa wamemzunguka Balozi aliyejeruhiwa

Naye msemaji wa baraza la maridhiano na ushirikiano ambaye alikuwa ndiye muandaaji wa mkutano huo, ameomba radhi kwa kutokuwa na ulinzi madhubuti .

Balozi Lippert, ni mshauri wa muda mrefu wa Raisi Obama na mambaye pia aliwahi kuwa msaidizi wa katibu mkuu wa ulinzi katika masuala ya mahusiano na bara la Asia,na alipata nafasi ya kuwa balozi Korea Kusini mwezi October mwaka wa jana.

Lippert amewahi pia kushika wadhifa wa afisa wa usalama wa taifa katika paresheni maalum na alitwaa medali ya nyota ya shaba nyeusi wakati alipoitembelea Iraq.

Korea Kusini na Kaskazini walitengana tangu mwaka 1950-53 baada ya vita vya Korea nab ado kiufundi wako vitani kwakuwa mapigano yalisitishwa kwa suluhu .

Marekani na Korea Kusini wameunganisha nguvu za kijeshi na wiki hii wako katika mazoezi kufuatia hali tata ya kiusalama kutoka kwa wakomunisti walioko Kaskazini .

Pyongyang wanadai kuwa wana fanya mazoezi kwa kujiweka tayari na uvamizi wowote utakao tokea wakati huo huo Korea Kusini na Marekani wao wanadai kuwa mazoezi yao ni kwa kujihami tu .

Marekani inakadiriwa kuwa na vikosi vya askari wake wapatao30,000 vya kudumu vilivyopiga kambi Korea Kusini.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company