Ukraine na waasi warudisha silaha zao nyuma

Picha ya Maktaba ikionyesha wanajeshi wa Ukraine.
Rais wa Ukraine, Petro Poroshenko, amasema waasi wanaoungwa mkono na Russia, wametoa sehemu kubwa silaha zao nzito kutoka mstari wa mbele wa mapambano mashariki mwa Ukraine.

Bwana Poroshenko, amesema yake imerudisha nyuma karibu silaha zake zote vile vile.

Kupitia televisheni ya taifa bwana Poroshenko, amesema mashambulizi yaliyogubika makubaliano ya wiki tatu ya kusitisha mapigano, yamepunguka kabisa.

Amesema wanajeshi 64 wa Ukraine, wameuwawa toka makubaliano ya kimataifa yalipotangazwa Febuari 15 huko Belarus.

Na katika tukio tofauti wizara ya ulinzi ya marekani Pentagon, ilitangaza kwamba vifaru 750 vya jeshi la nchi kavu la Marekani pamoja na magari ya vita na silaha nyenginezo zimewasili katika nchi ya Latvia.

Wanajeshi elfu 3 wamarekani wanatajariwa kupelekwa katika nchi hiyo.
CHANZO VOA SWAHILI
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company