Gabon mwenyeji wa michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika 2017

Shabiki wa timu ya soka ya Gabonwakati wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Afcon 2012.
AFP PHOTO / FRANCK FIFE
Na RFI

Gabon imechaguliwa kuandaa michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika katika mwaka 2017, shirikisho la soka barani Afrika CAF limetangaza Jumatano Aprili 8 mwaka 2015 katika mji mkuu wa Misri, Cairo.

Gabon ni moja ya nchi tatu ziliyokua zinagombea kwenye nafasi hiyo ya kuandaa michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2017. Gabon imechaguliwa dhidi ya Algeria na ghana. Libya ndio ingeliandaa michuano hiyo lakini iliomba iondolewe kwenye nafasi hiyo kutokana na kudorora kwa usalama na hali ya kisiasa ambayo imeendelea kusuasua.

Gabon itapokea michuano hiyo kwa mara ya pili, baada ya kushirikiana na nchi nyingine kuandaa michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2012.

Shirikisho la soka barani Afrika CAF limeichagua Gabon dhidi ya Ghana, ambayo imeshapokea michuano hiyo mara nne, pamoja na Algeria ambayo huenda imepoteza nafasi hiyo kutokana na hali ya usalama katika viwanja vyake, baada ya kifo cha mchezaji wa Cameroon, Albert Ebossé, Agosti 23 mwaka 2014.

Libya ambayo ingelipokea michuano hiyo, ilikua ilichaguliwa kupokea michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika katika mwaka 2013, lakini kutokana na vita viliyokua vikirindima wakati huo, iliomba ibadilishwe katika maandalizi ya michuano hiyo na iweze kuandaa michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2017.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company