Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuongeza zaidi fungu la fedha katika operesheni kudhibiti wahamiaji haramu, barani Ulaya.
Fedha hizo zitasaidia kusaka na kuokoa wahamiaji haramu katika bahari ya Mediterranean katika kudhibiti wimbi la wahamiaji hao wanaotaka kuingia Ulaya kutokea Afrika kaskazini.
Baada ya mazungumzo ya dharura mjini Brussels Ubelgiji viongozi hao pia wameidhinisha njia za kukamata na kuteketeza meli zinazoonekana kutumika katika biashara hiyo ya binadamu.
Nchi kadhaa za Ulaya zimeahidi kutoa meli, helikopta na nguvu kazi nyingine.
Kwa upande wake Rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk amesema ushirikiano mzuri unahitajika na nchi wahamiaji hao wanakotoka.BBC
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago