KUMEKUCHA JIMBO LA ISMANI LUKUVI APATA MPINZANI

MSOMI wa Digrii ya uhandisi wa kilimo na mtaalamu wa kilimo cha umwagiliaji kutoka chuo kikuu cha kilimo Sokoine (SUA)Mhandisi Sebastiani Kayoyo (39) anetangaza nia yake ya kugombea Ubunge katika jimbo la Isimani kwa tiketi ya CCM linaloshikiliwa na Waziri wa ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi Akitangaza nia yake hiyo mkoani Iringa juzi Kayoyo alisema kujitosa katika jimbo hilo ni kuhakikisha maendeleo yakiongezeka kwa kasi na kutoa fursa za kiuchumi kwa wananchi wa jimbo hilo.

Kayoyo alisema kuwa siko kwamba mbunge aliyeko madarakani hajafanya mambo ya msingi ila mbunge huyo ameongoza jimbo hilo kwa miaka mingi hivyo ni fursa ya hazina kubwa ya vijana walioko ndani ya chama cha mapinduzi kuweza kushika hatamu katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo katika nchii hiii "Mbunge anayeshikiria jimbo ninamheshimu sana na ameweza kufanya
mambo mengi mazuri, hivyo kwa kidemokrasia nina kuwa na Haki ya msingi kikatiba, nitahakikisha naendeleza mambo ya msingi ambayo bado
hajayatekeleza, hii ni pamoja na kuongeza nguvu kwa wananchi wengi waliokosa fursa mbalimbali" kayoyo.

Kakoyo ambaye kwa sasa ni mwajiriwa wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Rukwa kama muhandisi wa kilimo (Mtaalamu wa zana za kilimoba kilimo cha umwagiliaji )ni mzaliwa wa kijiji cha Tungamalenda kata ya idodi tarafa uya idodi iliyopo ndani ya Jimbo hilo la Isimani.

Alipoulizwa kuhusiana na hatima ya ajira yake endapo ataukosa ubunge ,”Mimi ni mtumishi wa serekalina ninajua raratibu zote za utumishi
serekali lakini niko tayari kuacha kazi ili kufanyakazi na ndugu zangu wa Isimani katika kujiletea maendeleo”
Akitaja vipaumbele vyake endapo chama chake kitampa ridha ya kukimbiza kijiti hicho Kayoyo alisema kuwa ataweka msisitizo katika
swala la afya , kilimo ,maji safi na salama pamoja na swala la miundombinu ikiwemo Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kwa kwa kuwa jimbo hilo halijawahi kuwa na lami tangu nchii hii ilipopata uhuru wake "Nia yangu ni kuona maendeleo ya jimbo hilo yakiongezeka, napenda
kuona wananchi ambao asilimia kubwa ni wakulima wakipata fursa za kusafirisha mazao yao nje ya jimbo hilo huku vijana nao wakipata
kuwezeshwa, uongozi ni kupokezana kijiti hivyo kijiti hicho nitakiongoza vizuri na naomba wananchi siku itakapofika ni kutekeleza wajibu" alisema Kayoyo.

Kwa kujitokeza huko kwa Kayoyo kunafanya idadi ya wagombea kutoka chama cha mapinduzi CCM kufikia wawili akiwemo Mbunge wa jimbo hilo, Wiliam Lukuvi ambaye bado ameonyesha nia ya kuendelea kuliongoza hukukwa upande wa chadema mbunge wa viti maamulu Chiku Abwawo pamojamakamu mwenyekiti wa bavicha Ole Sosopi
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company