12.00-Raia watakiwa kuendeleza maandamano Maandamano Burundi
Kiongozi wa kundi la kiraia linalopinga hatua ya rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu amewataka raia nchini humo kuendelea na maandamano kulingana na shirika la habari la AFP.
Vital Nshimiriman amesema kuwa licha ya kundi hilo kupinga jaribio hilo la mapinduzi,vile raia walivyowashangilia wanajeshi wa jaribio hilo kulionyesha kwamba kuna hamu kubwa ya mabadiliko.
10.30am-Majenerali waasi kushtakiwa
BurundiNukuu muhimu kutoka kwa Gervais Abayeho,msemaji wa rais Pierre Nkurunziza akizungumza na kipindi cha BBC cha Newsday.''Mapinduzi hushirikisha watu wengi Kuna wanajeshi wa nyadhfa za chini ambao wamesalimu amri na ambao wanawasaidia maafisa wa poisi na uchunguzi wao,lakini ninaamini watu waliopanga mapinduzi hayo ,wale viongozi hilo ni swala jingine ni lazima washtakiwe.hakuna mgawanyiko katika jeshi.Iwapo unaweza kuwaangalia wale waliokuwa wakipanga kutekeleza mapinduzi ni wachache ...kundi dogo la jeshi'',alisema..
10.00am-Majenerali waasi wakamatwa:
Maandamano yaliokuwa yakiendelea nchini Burundi dhidi ya rais Pierre NkurunzizaMajenerali wawili waliotekeleza jaribio la mapinduzi nchini Burundi dhidi ya rais Pierre Nkurunziza wamekamatwa.
Hatahivyo kiongozi wa mapinduzi hayo jenerali Godefroid Niyombare ametoroka na anasakwa kulingana na msemaji wa rais.
Awali Jenerali Niyombare alikiambia chombo cha habari cha AFP kwamba yeye na wafuasi wake watajisalimisha akiongezea kuwa ''natumai hawatatuua''.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amesema kuwa amerudi nchini Burund na kwamba anatarajiwa kulihutubia taifa.

