Mjadala wa Bangui wazua utata

Catherine Samba-Panza, rais wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wakati wa kutamatisha mjadala wa kitaifa wa bangui, Mei 11 mwaka 2015.
AFP PHOTO / PACOME PABANDJI
Na RFI

Sherehe za kutamatisha mjadala uliyowashirikisha raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kutoka tabaka mbalimbali zimefanyika Jumatatu wiki hii. Wakati huo huo milio ya risasi ilisikika mbele ya jengo la Bunge la mpito, huku kukionekana vizuizi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Bangui.
Katika Mkutano huo kulijadiliwa masuala nyeti. Baadhi ya walioshiriki mjadala huo wamepongeza masuali yaliyojadiliwa na hatua zilizofikiwa, huku wengine wakibaini kuwa mjadala huo umesababisha watu wengi kutoridhishwa kutokana na jinsi ulivyoendeshwa. Baadhi wamesema mjadala huo haukujikita na masuala nyeti yanayoikabili Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Katika hotuba yake, rais wa mpito Catherine Samba-Panza amekumbusha kwamba mkutano huo ulitajwa kuwa wa “ bahati ya mwisho “.

“ Kwa muda wa siku nane, raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamekutana kwa mazungumzo ya kitaifa, na kuafikiana katika masuala nyeti yanayolikabili taifa letu, hasa kuboresha maridhiano na kila mmoja kumsamehe mwenzake kwa yale aliyotendewa, lakini pia kutia saini kwenye mkataba wa kihistoria kati ya serikali na makundi hasimu yenye silaha, jambo ambalo limeifanya nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kufunua ukurusa mpya”,amesema Catherine Samba-Panza.

" Kipindi hiki cha mpito, sote tunakihitaji kituweke sawa, kuweko na amani, kwa kupelekea nchi yetu inarudi katika mfumo wa vyama vingi, mfumo ambao ni ishara ya kuanza kukua kidemokrasia. Shauku yangu ni kuona uchaguzi huu mkuu unafanyika mwishoni mwa mwaka kama tutachelewa ", ameongeza rais ais wa mpito.



Hata hivyo baadhi ya viongozi wa makundi hasimu ya Anti-balaka na Seleka wamefutilia mbali mjadala huo wa kitaifa. Kiongozi mmoja wa Anti-balaka alisikika akisema : “ nitawaomba viongozi wa serikali ya mpito kuzingatia maombi yetu na mapendekezo yetu”.

Kundi la wanamgambo wa Jamii ya Wakristo la Anti-balaka wanapendekeza kuachiliwa huru kwa wanamgambo wake wanaozuiliwa katika jela la Ngaragba. Pendekezo hilo limefutiliwa mbali na viongozi wa mashirika ya kiraia waliyoshiriki mjadala huo wa kitaifa mjini Bangui.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company