Tanzania yaadhimisha kumbukumbu ajali ya Mv Bukoba....watu takribani 1000 Walifariki Dunia

Mnara wa kumbukumbu ya eneo ambalo walizikwa watu waliopoteza maisha katika ajali ya MV Bukoba hiyo mnamo Mei 21.1996.

Leo ni tarehe 21 mei, siku ambayo kila mwaka watanzania wanaadhimisha tukio la ajali mbaya iliyowahi kutokea katika nchini iliyohusisha kuzama kwa meli ya MV Bukoba ndani ya ziwa Victoria. Leo ni miaka 19 tangu kutokea ajali hiyo

Ajali ya kuzama kwa Mv Bukoba ilitokea katika ziwa Victoria mnamo tarehe 21/5/1996 na kupoteza maisha ya zaidi ya watu takribani 1000 huku wengine wakizikwa katika kaburi la pamoja.

Mv Bukoba ilitengenezwa mwaka 1979 na ilikuwa na uwezo wa kubeba mizigo ya Tani 850 na wasafiri 430. Inakadiriwa katika ajali iyo watu kufikia 1,000 walipoteza maisha.

Mtandao wa Mpekuzi unaungana na watanzania wote kuwaombea wote waliofariki dunia katika ajali hiyo.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company