Uhusiano wa Bin Laden na Aqmi pamoja na Al Shebab

Osama Bin Laden alionekana katika video hii, iliyokamatwa na Pentagon Mei 7 2011.
REUTERS/Pentagon/Handout
Na RFI

Uhusiano wa Osama Bin Laden ulikua muhimu kwa tawi la kundi hilo katika ukanda wa Afrika Madharibi Aqmi. Idara ya ujasusi ya Marekani CIA imeweka wazi wiki hii nyaraka 103 ziliyopatikana katika Jumba la Abbottabad, nchini Pakistan Pakistan, ambapo majeshi maalum ya Marekani yalifanikiwa kumuua kiongozi huyo wa wa kundi la kigaidi la Al Qaeda.

Kumegunduliwa katika nyaraka hizi kuwa Bin Laden alikuwa akifuatilia kwa karibu harakati za kundi la Aqmi lenye mafungamano na Al Qaeda, na alikua akitoa nasaha kwa kundi la wanamgambo wa Al Shabab.

Katika barua kadhaa ziilyogunduliwa katika jumba hilo, Bin Laden alikua akiwapa mafunzo viongozi wa kundi la Aqmi. Bin Laden alikua akiwasihi viongozi hawa kutojidanganya kwa adui. " Tuliamua kuanzisha harakati zetu katika ukanda wa Afrika Madharibi ili kuvunja nguvu za adui yetu mkuu kwa kushambulia balozi za Marekani katika bara la Afrika ".

Alitoa mfano wa balozi za Marekani ziliopo Sierra Leone na Togo, ambazo hazimo moja kwa moja katika eneo ambalo Aqmi inaendeshea harakati zake.

Katika barua hiyo isiyo na tarehe, Bin Laden alikua aliwapa nasaha viongozi wa Aqmi ya kufanya mashambulizi dhidi ya makampuni ya mafuta ya Marekani. Bin Laden aliendelea kusema " lengo letu ni lakung'oa mti wenye chuki na sisi hasa tukianzia kwenye shina ambalo ni Marekani". Marekani bado ni moja ya nchi zinazolengwa na makundi hayo.

" Utaratibu si kushambulia adui wa ndani, isipokuwa katika hali ambapo doria wake au vikosi vya usalama na ulinzi vya moja ya nchi z za ukanda wa Afrika Magharibi watashambulia ngome za ndugu zetu", alisisitiza Bin Laden.

Hakuna barua au hata moja miongoni mwa barua hizo iliyowasilishwa kwa kundi la Aqmi.

■ Nasaha za Bin Laden kwa wanamgambo wa Al Shabab

Katika barua ya tarehe 7 Agosti, Bin Laden anaeleza hali ya Somalia na anaagiza mapendekezo kadhaa kwa wanamgambo wa kundi la Al Shabab ya kutowatenganisha wananchi. Ahmed Godane, kiongozi wa Al Shabab, aliwahi kumuandikia barua Osama Bin Laden, akimuomba kundi lake kujiunga na Al-Qaeda, jambo ambalo Osama Bin Laden alipinga.

Wakati huo Bin Laden alitoa nasaha kwa kundi la wanamgambo wa Al Shabab ya kutowatenganisha na kuwashambulia wananchi.

Bin Laden Aliwasihi wsanamgambo wa Al Shabab kutowatenga na kuwafanyia vibaya watu kutoka jamii ya Wasufi, ili wasiwezi kukimblia mikononi mwa adui. Wakati huo nchini Somalia maeneo takatifu ya jamii hiyo yalishambuliwa na kiongozi wao kuuawa.

Bin Laden aliwasihi pia wanamgambo wa Al Shaba kutoendesha mashambulizi dhidi ya makao makuu ya kikosi cha wanmajeshi wa Umoja wa Afrika nchini Somalia Amisom, kwa kuepuka ulipizaji kisase wa wanajeshi hao kwenye soko la Bakara, ambapo raia wengi wa kawaida walikua wakiuawa.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company