KIGOMA WATAKA UZINDUZI WA ALBAMU TATU ZA MWAITEGE

WAKAZI wa Mkoa wa Kigoma, wameiomba Kampuni ya Msama Promotions kuwapelekea uzinduzi wa albamu tatu za mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili nchini Boniface Mwaitege.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama amepokea maombi mengi kwa wakazi wa mkoa huo wakihitaji uzinduzi huo ufanyike mkoani kwao.

“Nimepokea maombi ya wakazi wa Kigoma wakihitaji uzinduzi wa muimbaji nguli, Bonny Mwaitege ambaye anatarajia kuzindua albamu tatu,” alisema Msama.

Msama alisema mbali ya Kigoma mikoa mingine imeonesha nia ya kutaka uzinduzi huo ufanyike mikoani kwao.

Alisema wakazi wa Kigoma wanatamani kumuona akifanya onyesho mkoani humo kwa kuwa ni moja ya waimbaji ambao wamekuwa wakiwashuhudia wakifanya makubwa jukwaani.

Aidha Msama alisema kuwa kujitokeza kwa baadhi ya wananchi wa mikoa mbali hiyo kuomba, inampa moyo kuona watu wamemgeukia Mungu na kutaka kupata neno kutoka kwa waimbaji wa muziki wa injili ambako alisistiza kuwa yuko pamoja nao na atajitahidi.

Mwimbaji huyu machachari ambaye anatamba na nyimbo mbalimbali kama Mama ni mama, Mke mwema, Wakusamehe, fungua moyo wako na njoo uombewe na Yesu yupo anatarajia kuzindua albamu hizo tatu Agosti 2 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Msama alisema kuwa Kamati ya Maandalizi itaketi na kujadili kwa sababu ni mikoa mingi iliyoomba kupelekewa uzinduzi huo hivyo ni jambo la kujipanga kuona namna itakavyoweza kufanya na kuwafikia katika mikoa yao.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company