Mvutano wajitokeza kati ya Maseneta wa Marekani

NSA hawezi, hadi itakapotangazwa tena, kufanya udukuzi au kuchunguza mamilioni ya watu wanaoongea kwa simu, kwa ajili ya usalama wa taifa. mawasiliano kadhaa ya simu zisizo salama ya John Kerry yalisikilizwa.
REUTERS/Lucas Jackson
Na RFI

Maseneta nchini Marekani wameshindwa kuafikiana kuhusu sheria mpya ya kuwaruhusu maafisa wa ujajusi kuchunguza na kusikiliza mawasiliano ya simu katika harakati za kuimarisha usalama.

Hii inamaanisha kuwa maafisa wa ujajusi nchini humo hawawezi kwa sasa kuchunguza mawasiliano ya simu ya watu nchni humo kuhakikisha kuwa nchi hiyo inakuwa salama.

Hatua hiyo imeikasirisha serikali ya Marekani ambayo inasema Maseneta hao wanaweka hatarini usalama wa nchi hiyo wakati huu sheria hiyo mpya ikisubiriwa kujadililiwa tena katikati ya juma hili.

Shirika la kijasusi la NSA tayari limefunga mitambo yake ya kuchunguza mawasiliano hayo baada ya Maseneta kushindwa kukubaliana.

Kinachowagawa wanasiasa hao ni suala la uhuru wa watu kuwasiliana, kuna baadhi wanosisitiza kuwa mswada huo unaweza kupitsihwa tu baada ya mswada mwingine unaozungumzia uhuru kupitishwa.
   Baraza la Seneti wiki hii litaendelea kuchunguza kazi iliofanyika huku likimuomba Rand Paulo kutochelewesha mchakato kwa muda mrefu sasa pamoja na upatikanaji wa idadi kubwa ya maseneta, Republican na Democrats, wanaomuunga mkono.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company