Rais wa Sudan, Omar Al-Bashir ameondoka Afrika Kusini, baada ya Mahakama ya Pretoria kumba serikali ya Afrika Kusini kumzuia ili asiwezi kuondoka na asafirishwe hadi kwenye ICC.
REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Na RFI
Baada ya Mhakama ya Pretoria kuchukua uamzi wa kuitaka serikali ya Afrika Kusini kumzuia rais Sudani ili asiwezi kuondoka nchini humo, hatimaye Omar Al-Bashir amewasili jijini Kharoum.
Ubalozi wa Sudan nchini Afrika Kusini umefahamisha kwamba rais Omar Al-Bashir ameondoka nchini Afrika Kusini Jumatatu mchana Juni 15. Vyombo vya habari vya Afrika Kusini vimebaini kwamba vimeona ndege ya rais wa Sudan ikipaa hewani ikitokea kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi wa Johannesbourg.
Vyombo hivyo vya habari vimepiga hata picha ya jinsi ndege hiyo ya rais ikipaa hewani. Taarifa hii imethibitishwa na serikali ya Khartoum. Waziri wa habari, Yasser Youssef, amelielezea shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba “ ndege ya rais Bashir imeondoka Johannesbourg Alaasiri”.
Rais Omar Al-Bashir alijielekeza juma lililopita nchini Afrika Kusini kuhudhuria mkutano wa 25 wa Umoja wa Afrika ambao ulifunguliwa Jumapili Juni 14 jijini Johannesburg. Zaidi ya marais hamsini walihudhuria mkutano huo.
Awali Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita (ICC) iliiomba serikali ya Afrika Kusini kumzuia rais wa Sudan Omar al-Bashir, ambaye anatuhumiwa na Mahakama hiyo makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu na mauaji ya kimbari katika vita viliyotokea Darfur.
Mahakama ya Afrika Kusini, iliombwa na shirika lisilo la kiserikali la Southern Africa Litigation Center, kumzuia rais wa Sudan ili asiwezi kuondoka nchini humo, angalau mpaka Jumatatu wiki hii.
Shirika hilo limeiomba Mahakama ya Afrka Kusini kumzuia rais Omar al-Bashir na kumsafirisha hadi kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita (ICC). Kufuatia ombi hilo, Mahakama ya Pretoria ilikua ilimzuia rais wa Sudan kutothubutu kuondoka nchini Afrika Kusini mpaka vyombo vya sheria vitoe uamzi wake wa mwisho.
Kesi hiyo imeahirishwa kusikilizwa hadi kesho Jumatatu asubuhi kwa ombi la wakili wa serikali wa Afrika Kusini, ambaye anahitaji kuandaa hoja yake kwa ajili ya kikao cha pili.
Waziri ya mambo ya ndani wa Afrika Kusini alikua ametakiwa kufuatilia kwa karibu maeneo yote hususan mipaka ambapo rais Omar al-Bashir anaweza kupitia kwa kuondoka nchini Afrika Kusini usiku wa Jumapili mwishoni mwa juma hili lililopita.
Omar Al-Bashir amelakiwa na maelfu kwa mamia ya wafuasi wake alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kharthoum.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago